VETA yafadhili mafunzo kwa wanawake 3000 jijini Dodoma

Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imetoa ufadhili wa mafunzo ya muda mfupi kwa wanawake 3000 jijiji Dodoma, yatakayotolewa katika Chuo cha VETA Dodoma.

Akizungumza jana, tarehe 24 Machi, 2025 wakati wa hafla ya uzinduzi wa mafunzo hayo yanayotolewa kupitia kikundi cha Wanawake na Samia, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amemshukuru Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore kwa ufadhili wa mfunzo hayo.

Senyamule amesema wanawake wengi, hawana ujuzi, hivyo mafunzo ya stadi kwao ni muhimu ili kuwawezesha kujiajiri au kuajiriwa.

“Dodoma sasa ni mji wa kitalii na watu wengi wanakuja kwa ajili ya kupata huduma sa Kiserikali. Wapo wengine kutoka mataifa mbalimbali. Hivyo tunahitajika kutoa huduma za kiwango cha kimataifa na hilo linawezekana ikiwa tutapata mafunzo,” amesema Senyamule.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma, Fatuma Madidi ametoa pongezi kwa Mkurugenzi Mkuu wa VETA na Mkuu wa chuo cha VETA Dodoma kwa kuridhia mafunzo hayo kutolewa kwa wanwake wa Dodoma kupitia chuo cha VETA Dodoma.

“Ukimsomesha mwanamke umesomesha jamii nzima, tunaahidi kuwa watulivi na kujifunza kwa bidii,” amesema Madidi.

Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Kasore amesema VETA itagharamia mafunzo hayo kwa wanawake na Samia na kuongeza kuwa anaamini ujuzi watakaoupata utawasaidia kuendesha shughuli zao za uzalishaji na kujingiizia kipato.

spot_img

Latest articles

Oktoba 29 siku ya giza, ifungue milango ya haki

OKTOBA 29, 2025 itabakia kuwa siku ya giza na machungu katika historia ya Jamhuri...

Fountain Gate yatoa kocha bora

Na Mwandishi Wetu Kocha wa timu ya Fountain Gate,  Mohamed Laizer amechaguliwa kuwa kocha bora...

Nyota JKT Queens aipigia hesabu Asec Mimosa

Na Winfrida Mtoi Mshambuliaji wa JKT Queens FC, Jamila Rajabu, amesema  amejipanga  kutengeneza  nafasi na...

Zungu achaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Na Mwandishi Wetu MBUNGE mteule wa Jimbo la Ilala Mussa Azzan Zungu ameibuka mshindi...

More like this

Oktoba 29 siku ya giza, ifungue milango ya haki

OKTOBA 29, 2025 itabakia kuwa siku ya giza na machungu katika historia ya Jamhuri...

Fountain Gate yatoa kocha bora

Na Mwandishi Wetu Kocha wa timu ya Fountain Gate,  Mohamed Laizer amechaguliwa kuwa kocha bora...

Nyota JKT Queens aipigia hesabu Asec Mimosa

Na Winfrida Mtoi Mshambuliaji wa JKT Queens FC, Jamila Rajabu, amesema  amejipanga  kutengeneza  nafasi na...