UPOTEVU WA MAJI WASABABISA HASARA YA SH 114.12 BILIONI

Na Mwandishi Wetu

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko amezielekeza mamlaka za maji kupunguza kiwango cha upotevu maji ili kuepusha hasara ya sh 114.12 bilioni  iliyotokana na upotevu huo kwa mwaka huu.

Dk. Biteko amesema hayo jijini Dar es Salaam Machi 19, 2025 wakati akizindua  taarifa ya Utendaji wa Mamlaka za maji kwa mwaka 2023/24 na kusema upatikanaji wa huduma za maji ni haki ya msingi hivyo ni muhimu kulinda vyanzo vya maji kuwezesha upatikanaji wake.

Amesema pamoja na jitihada zinazoendelea jamii ina wajibu wa kuhakikisha usafi wa mazingira, kupanda miti na kuhifadi misitu ili kuendelea kupata na kutumia rasilimali maji.

“Tusipotunza vyanzo vya maji na kuhifadhi mazingira tutajikuta katika mtanziko mkubwa (water Stress),” amesema na kuongeza kuwa kukosekana kwa rasilimali maji kwa baadhi ya watu kinaweza kuwa chanzo cha migogoro na machafuko katika jamii husika.

Amesema hadi sasa asilimia 84 kwa mijini na asilimia 79.6 kwa maeneo ya vijijini zimeunganishwa na huduma ya maji ambapo kuna ongezeko la asilimia 7 kutoka kipindi cha mwaka uliotangulia.

Awali, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema kumekuwa na ongezeko la ubora wa viwango vya maji na udhibiti wa upotevu wa maji ambao unasababisha hasara kubwa hasa unapothamanishwa kifedha.

Hata hivyo ameipongeza EWURA kwa kazi nzuri na kutoa taarifa inayoonesha uhalisia wa mambo huku akisema mamlaka zinazofanya vizuri zinapata tuzo ikiwa ni motisha ya ushindani wa kimaendeleo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya EWURA, Profesa Mark Mwandosya ameipongeza Serikali kwa kuendelea kutoa kipaumbele na kuongeza bajeti ambayo imeongezeka kutoka sh 206 bilioni  mwaka 2010/11 hadi sh 558 bilioni  mwaka 2024/25

Amesema uwekezaji wa katika sekta ya maji unaleta faida zaidi ya mara saba ya mtaji ambapo uwekezaji wa dola 1 unaweza kuleta faida ya dola 7 katika uchumi wa taifa.

Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Dk. James Andelile amesema pamoja na mafanikio yaliyofikiwa bado kuna changamoto kadhaa zinazotokana na utegemezi wa Mamlaka za maji kwa Serikali.

Pia amesema changamoto nyingine ni uchakavu wa miundombinu ya maji inayosababisha upotevu wa maji na hasara kwa serikali.

Mamlaka za maji zilizofanya vizuri katika udhibiti wa upotevu wa maji na asilimia ya maji yanayopotea ni Maganzo 4%, Nzega 6%, Kashuwasa 11%, Biharamulo 12% na Mwanuzi 13%.

Mamlaka zilizoshindwa kudhibiti upotevu huo kwa kiwango kikubwa ni Rombo 70%, Handeni 69%, Mugango/kyabakari 68%, Ifakara 56% na Kilindoni 55%.

spot_img

Latest articles

Upanuzi wa Kituo cha Kupoza umeme Mbagala mbioni kukamilika

📌Awamu ya kwanza ya upanuzi wa Kituo Megawati 45 yakamilika 📌Asema wananchi wa Mbagala...

Rais Samia aeleza mambo ya kujifunza kutoka kwa Hayati Cleopa Msuya

Na Mwandishi Wetu Rais Samia Suluhu Hassan ameongoza mazishi ya aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa...

TFF yamfungia miaka sita Katibu Mkuu DRFA

Na Mwandishi Wetu Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA),Ramadhan...

Jeshi la Polisi lamkamata kiongozi wa Chadema

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limemkamata Naibu Katibu Mkuu...

More like this

Upanuzi wa Kituo cha Kupoza umeme Mbagala mbioni kukamilika

📌Awamu ya kwanza ya upanuzi wa Kituo Megawati 45 yakamilika 📌Asema wananchi wa Mbagala...

Rais Samia aeleza mambo ya kujifunza kutoka kwa Hayati Cleopa Msuya

Na Mwandishi Wetu Rais Samia Suluhu Hassan ameongoza mazishi ya aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa...

TFF yamfungia miaka sita Katibu Mkuu DRFA

Na Mwandishi Wetu Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA),Ramadhan...