Ajali yasababisha kifo cha SP Awadh

Na Mwandishi Wetu 

MKUU wa Polisi Wilaya ya kipolisi Chanika, Awadhi Chico amefariki dunia baada ya kupata ajali maeneo ya Pugu mwisho wa lami jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Machi 17, 2025 na Kaimu Kamanda Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Fausine Mafwele imeeleza kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa 1:20 asubuhi ambapo magari mawili yaligongana na kusababisha kifo cha mtu mmoja na majeruhi mmoja.

“Ajali hiyo imetokea baada ya dereva wa Daladala yenye usajili namba T 580 EAE aina ya TATA inayofanya safari zake kati Zingiziwa Chanika na Machinga Complex Ilala akitokea Pugu kwenda Gongo la Mboto iligongana na gari T 952 AMD aina ya Toyota Prado iliyokuwa ikiendeshwa na PF 15950 SP Awadh Mohamed Chico ambaye ni mkuu wa Polisi wilaya ya kipolisi Chanika akitokea Gongo la Mboto kuelekea Pugu na kusababisha kifo chake hapohapo.

“Pia kusabisha majeraha kwa WP 5616 Cpl Zubeda Ramadhani Sadala wa wilaya kipolisi Chanika aliye kuwa abiria kwenye gari namba T952 AMD ambaye amevunjika mkono wa kushoto,” amesema.

Amefafanua kuwa, chanzo cha ajali hiyo ni baada ya dereva wa daladala kuyapita magari yaliyokua mbele yake bila kuchukua tahadhari na kusababisha kungongana uso kwa uso.

“Jeshi la Polisi linamtafuta dereva wa daladala ambaye hajafahamika aliyetoroka baada ya kusababisha ajali hiyo. Pia Jeshi la Polisi kanda Maalum Dar es Saalam linakanusha taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya Habari Nchini kuwa aliyefariki ni Kamishina wa Operasheni na Mafunzo Tanzania CP Awadhi Juma Haji,” amesema.

Aidha amesema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa taarifa zilizokuwa zinasambaa katika mitandao ya kijamii zinazodai kuwa Faraja Samweli Ng’andu (28) mkazi wa msongola akiwa na Watoto wake wawili Nathanael John Mtulia (4) na Beyonce John Mtulia (3) wameuwa.

“Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa mwanamke huyo aliondoka nyumbani kwake tarehe 12/03/2025 majira ya saa 5:00 asubuhi kutokana na kuwa na mgogoro wa ndoa na mume wake aitwaye John Gabriel Mtulia (33) mkazi wa Msongola Chanika Dar es salaam ambaye alieleza kuwa walihitilifiana na mke kwa muda mrefu na kusababisha kuondoka kwenda kwa wazazi wake wanaoishi maeneo ya kipunguni ‘’B’’.

“Ambapo tarehe 02/03/2025 alirudi nyumbani kwa mume wake na kumuomba msamaha kuwa ana ujauzito ambao sio wa kwake ni wa mwanaume aitwaye Maliki mwingine na kwamba hawezi kuendelea kuishi tena na mume wake baada ya hapo waliendelea kuishi pamoja,” amesema na kuongeza kuwa:

“Tarehe 12/03/2025 Faraja Samweli aliamua kuondoka nyumbani kwa kutumia bodaboda aliyokodi ikiendeshwa na Ramadhani Pondamali ambaye alimpeleka na kumshusha maeneo ya kisima cha mafuta ya GPB iliopo uwanja wa ndege wa Julius Nyerere baada hapo alipanda bajaji ambayo ilimpeleka kusikojulikana mpaka sasa mwanamke huyo anaendelea kutafutwa,”.

Vilevile, Jeshi la polisi limetoa wito kwa wananchi kuwa pmoja na barabara nyingi za jiji kuwa katika matengenezo kufuata sheria za ssalama barabarani ili kuepuka kutokea kwa ajali.

spot_img

Latest articles

Waziri Aweso: Tuna uhakika wa maji ya kutosha Dar na Pwani

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amewatoa hofu wakazi wa mikoa ya...

PURA yajivunia mafanikio katika Ajenda ya Nishati Safi na ushiriki wa Watanzania Sekta ya Mafuta na Gesi

Na Tatu Mohamed MAMLAKA ya Kudhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imesema inajivunia...

Machungu, damu yamwagwa tena

Maadhimisho ya Saba Saba nchini Kenya ni tukio muhimu katika kukumbuka mapambano ya kudai...

eGA yatumia Sabasaba kuelimisha umma kuhusu Mfumo wa e-Mrejesho, yajivunia Tuzo ya Kimataifa

Na Tatu Mohamed MAMLAKA ya Serikali Mtandao (eGA) imeendelea kuonesha namna ambavyo Serikali inavyotekeleza mageuzi...

More like this

Waziri Aweso: Tuna uhakika wa maji ya kutosha Dar na Pwani

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amewatoa hofu wakazi wa mikoa ya...

PURA yajivunia mafanikio katika Ajenda ya Nishati Safi na ushiriki wa Watanzania Sekta ya Mafuta na Gesi

Na Tatu Mohamed MAMLAKA ya Kudhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imesema inajivunia...

Machungu, damu yamwagwa tena

Maadhimisho ya Saba Saba nchini Kenya ni tukio muhimu katika kukumbuka mapambano ya kudai...