VETA yapaka rangi jengo la Watoto MNH

Na Tatu Mohamed

KATIKA kuadhimisha miaka 30 tangu ilipoanzishwa, Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imepaka rangi katika jengo la Watoto la Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Katika hafla hiyo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, ambaye alikua mgeni ameeleza kufurahishwa na mabadiliko makubwa yaliyofanyika Muhimbili na kusisitiza umuhimu wa kushirikiana katika kuboresha huduma za afya nchini.

“Tunawashukuru VETA na Coral Paints kwa kutoa rangi. Sisi tunathamini kazi inayofanywa na Muhimbili na tunaendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais wa Samia Suluhu Hassan katika kuboresha sekta ya Afya.

“Rangi hii inapakwa na vijana wetu wa VETA ambao wamekuja hapa kuonesha uwezo wao waliosomea katika vyuo vyetu,” amesema.

Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Antony Kasore, amesema kuwa msaada huo ni sehemu ya dhamira ya VETA ya kurudisha kwa jamii.

“Katika kuadhimisha miaka 30 ya VETA, tuliona ni muhimu kushiriki katika miradi inayogusa maisha ya wananchi moja kwa moja. Kupaka rangi Jengo la Watoto hapa Muhimbili ni moja ya njia za kuonyesha kuwa kile tunachofundisha kina tija kwa jamii. Tunaamini kuwa mazingira safi na yenye mvuto yanaweza kusaidia watoto waliolazwa kupata ahueni haraka,” amesema Kasore. 

Kwa upande wake, Dkt. Faraja Chiwanga, aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa MNH ameeleza kuwa hospitali hiyo ni kubwa yenye mahitaji mengi yanayohitaji rasilimali nyingi hivyo kupata msaada kutoka VETA na wadau wengine ni jambo muhimu linalopaswa kupongezwa.

“Zamani, tulikuwa tunaamini kuwa hospitali ni mahali pa tiba tu, lakini sasa tunajua kuwa mazingira nayo yana mchango mkubwa kwa afya na ustawi wa wagonjwa, hususan watoto, tunapenda hospitali yetu iwe mahali ambapo watoto wanapokuja, wasijisikie kama wako kwenye mazingira ya hofu, bali wajione wako sehemu salama na yenye faraja,” amesema Dkt. Chiwanga.

Naye, Meneja Masoko wa Kampuni Insignia Limited ambao wanatengeneza rangi za Coral Paints, Adam Kefa amesema kampuni yake kupitia bidhaa zake za rangi bora imekuwa ikisaidia jamii katika maeneo mbalimbali, ikiwemo sekta ya afya.

”Ni faraja kwetu kushirikiana na VETA kutoa msaada huu kwa watoto njiti, ambao ni sehemu ya tarajio la nchi katika kukuza uchumi hapo baadae,”

”Rangi hizi tulizozitoa, mbali ya kukarabati majengo ya wodi za watoto, pia zitasaidia kukuza akili zao kwa sababu rangi siku zote zinavutia kwa watoto na kuwapa furaha muda wote,” amesema Kefa.

spot_img

Latest articles

Kikwete mgeni rasmi kongamano la PBA kesho

Na Mwandishi Wetu RAIS Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikkwete anatarajiwa kuwa...

Mwanza journos sharpen skills for upcoming elections

By Our Correspondent, Mwanza The Resident Representative of the non-governmental organization Konrad Adenauer Stiftung (KAS)...

Wanahabari Mwanza wafundwa kuhusu Sheria za Uchaguzi, maadili

MWAKILISHI Mkazi wa shirika lisilo la kiserikali la Konrad Adenauer Stiftung nchini, Peter Koch,...

Wanahabari Mwanza wafundwa kuhusu Sheria za Uchaguzi, maadili

Na Mwandishi Wetu, Mwanza MWAKILISHI Mkazi wa shirika lisilo la kiserikali la Konrad Adenauer Stiftung...

More like this

Kikwete mgeni rasmi kongamano la PBA kesho

Na Mwandishi Wetu RAIS Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikkwete anatarajiwa kuwa...

Mwanza journos sharpen skills for upcoming elections

By Our Correspondent, Mwanza The Resident Representative of the non-governmental organization Konrad Adenauer Stiftung (KAS)...

Wanahabari Mwanza wafundwa kuhusu Sheria za Uchaguzi, maadili

MWAKILISHI Mkazi wa shirika lisilo la kiserikali la Konrad Adenauer Stiftung nchini, Peter Koch,...