Mkenda: Tutaendelea kuimarisha ushirikiano sekta ya nguo na mavazi

Na Tatu Mohamed

SERIKALI imesema itaendelea kuimarisha ushirikiano kati yao, viwanda na wabunifu ili kufanikisha maendeleo katika sekta ya nguo na mavazi.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, katika Kongamano la kujadili maendeleo na changamoto zinazoikabili sekta hiyo lililoandaliwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), kuelekea maadhimisho ya miaka 30.

Amesema asilimia kubwa ya wanaojihusisha katika sekta hiyo hawana kiwango kikubwa cha elimu lakini wanao ujuzi na ubunifu mzuri katika kutengeneza bidhaa zinazovutia.

“Tunawahitaji sana katika kuimarisha ujuzi tunaoutaka, kwani itawasaidia wanafunzi wetu kujifunza kwa vitendo kupitia nyinyi. Naipongeza VETA kwa kuandaa kongamano hili, na endeleeni kujenga mahusiano mazuri na wadau hawa muhimu.

“Ndoto ya serikali na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha tunazalisha bidhaa zenye ubora kwa wingi ili tuuze ndani na nje ya nchi,” amesema Profesa Mkenda.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore amesema lengo la kongamano hilo ni kukutana na kujadili namna VETA inaweza kushirikiana na wadau hao ili kuendeleza sekta hiyo.

“Mada mbalimbali zimewasilishwa katika kongamano hili na katika kujadiliana tumeona wadau ni wengi na soko ni kubwa, hivyo tunatakiwa kulitumia ili kuzalisha bidhaa za kutosha,” amesema.

Mbunifu wa Mavazi, Miriam Ekilwa amesema: “Tunafurahi hatua ya serikali kutambua umuhimu wetu. Ni matarajio yetu ushirikiano huu unafanyika kwa vitendo ili kuikuza sekta hii muhimu,”.

spot_img

Latest articles

Kibabage aimpa mzuka Serengeti Boys kuelekea fainali ya AFCON

Na Winfrida Mtoi BEKI wa timu ya Taifa (Taifa Stars), Nickson Kibabage amesema kitendo cha...

Aishi Manula afunguka ugumu wa kuikabili Uganda

Na Winfrida Mtoi Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), imeanza mazoezi kujiandaa na michezo...

‎Msigwa: Bwawa la Kidunda ni mradi wa kimkakati kwa Maji, Kilimo na Nishati

Na Mwandishi Wetu Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, ameipongeza Wizara ya Maji kwa...

DAWASA yafafanua sababu ya ukosefu wa maji maeneo ya Kibaha hadi Kisarawe

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)...

More like this