TEF kufanya Mkutano Mkuu Maalum wa kuchagua viongozi wapya

Na Mwandishi Wetu 

JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF) limeandaa Mkutano Mkuu Maalum wa wanachama wake wote, ambao umepangwa kufanyika Aprili 3-5, 2025, katika Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma. 

Mgeni rasmi katika mkutano huo wenye kauli ya ‘Uchaguzi Huru na wa Haki’ anatarajiwa kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mgombea Mwenza wa nafasi ya Makamu wa Rais wa CCM kwa mwaka 2025, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Machi 07, 2025 na Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile imeeleza kuwa, Mkutano huo ni kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa viongozi kwa kuzingatia Ibara ya 7.8 ya Katiba ya TEF, ambapo muda wa uongozi wa sasa unafikia tamati mwaka huu, baada kuwapo madarakani kwa miaka minne tangu Mei 2021.

“Tunatarajia kwamba Balozi Nchimbi, atafungua Mkutano huu, Aprili 4, 2025 na uchaguzi wa Viongozi wa TEF utafanyika Aprili 5, 2025,” imeeleza taarifa hiyo.

Imebainisha kuwa nafasi ambazo viongozi wake watapigiwa kura kwa mujibu wa Katiba ni tisa (9) ambao ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe saba wa Kamati ya Utendaji (KUT) ya TEF.

“Fomu za kuomba nafasi za uongozi zitaanza kutolewa rasmi Jumatatu Machi 10, 2025 kwenye Ofisi za TEF. Siku ya mwisho ya kuchukua na kurejesha fomu itakuwa ni Jumatatu ya Machi 24, 2025, saa 10:00 jioni. 

“Mgombea atarejesha fomu pamoja na picha ndogo (passport size) ambayo itatumika kwenye karatasi ya kura ikiwa atateuliwa kuwania nafasi anayoomba. Muda wa kuchukua na kurejesha fomu ni kuanzia saa 03:00 asubuhi – 10:00 jioni kwa siku za kazi. Hii inamaanisha kwamba fomu hazitatolewa wala kupokelewa Jumamosi, Jumapili wala siku za Sikukuu,” imeeleza taarifa hiyo.

Imefafanua kuwa, ada ya fomu za uongozi ni Sh.150,000 kwa nafasi za Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti na Sh.100,000 kwa nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji.

“Utoaji na urejeshaji wa fomu za kuomba uongozi utasimamiwa na Sekretatieti ya Jukwaa la Wahariri (TEF) chini ya Ofisa ya Mtendaji Mkuu. Kamati ya Uchaguzi itaongozwa na Frank Sanga (Mwenyekiti) na wajumbe wengine wawili ambao ni Angela Mang’enya na Rashid Kejo.

“Kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za TEF, Kamati hii ndiyo yenye wajibu wa kuhakikisha taratibu zote zinafuatwa ikiwa ni pamoja na vigezo na sifa za wagombea. Tunashauri wanachama wote na hasa wale wenye nia ya kugombea nafasi za uongozi, wasome Kanuni za Uchaguzi na kuzielewa,” imeeleza taarifa hiyo.

spot_img

Latest articles

Baraza la saba la Wafanyakazi Wizara ya Nishati lakutana Dodoma

📌 Dkt. Kazungu asema Wizara itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya Kimkakati 📌 Baraza lapitisha rasimu...

Wizara ya Nishati yataja mafanikio utekelezaji majukumu 2024/25

📌 Uzalishaji umeme waongezeka kwa asilimia 59.9 📌 Misheni 300 kuongeza upatikanaji umeme...

Gavana Tutuba: Hali ya uchumi wa Tanzania inaendelea kuimarika

Na Tatu Mohamed GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba amesema kuwa, hali...

Dkt. Biteko: Ufundi Stadi umepewa kipaumbele na serikali

📌 Asisitiza kuwa, Rais Samia anajenga vyuo kila wilaya nchini 📌 Apongeza utoaji wa mafunzo...

More like this

Baraza la saba la Wafanyakazi Wizara ya Nishati lakutana Dodoma

📌 Dkt. Kazungu asema Wizara itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya Kimkakati 📌 Baraza lapitisha rasimu...

Wizara ya Nishati yataja mafanikio utekelezaji majukumu 2024/25

📌 Uzalishaji umeme waongezeka kwa asilimia 59.9 📌 Misheni 300 kuongeza upatikanaji umeme...

Gavana Tutuba: Hali ya uchumi wa Tanzania inaendelea kuimarika

Na Tatu Mohamed GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba amesema kuwa, hali...