Makalla: Lazima uchaguzi ufanyike kwa mujibu wa Katiba na Sheria

Na Mwandishi Wetu

KATIBU wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla amesema Uchaguzi Mkuu mwaka wa huu 2025 utafanyika kwa mujibu wa katiba na sheria kwani mabadiliko yameshafanyika, hivyo hakuna atakayezuia uchaguzi.

CPA. Makalla ameeleza hayo leo Machi 4, 2025 wakati akizungumza katika Mkutano wa Viongozi wa Chama na Jumuiya ngazi ya Shina, Tawi, Kata na Wilaya katika Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es salaam, ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tano katika mkoa huo.

“Uchaguzi utafanyika kwa mujibu wa katiba kwa mujibu wa sheria, nimeona kwenye magroup yao wanaambiana wachangiane tone kwa tone tuchangiane tuende kwenye nguvu ya umma kuzuia uchaguzi, hela zitaliwa kwa sabaau uchaguzi utafanyika,” amesema Makalla.

Akizungumza na Viongozi hao CPA. Makalla ameongeza kuwa kama watabaki na msimamo wao wa kutoshiriki uchaguzi ni dhahiri baada ya uchaguzi mkuu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hakitokuwa na nguvu ya kuendelea kuwa chama kikuu cha upinzani nchini, kwani kwa kufanya hivyo kitaua ndoto za wengi wenye ndoto za kugombea udiwani, ubunge na viti maalumu kwani uongozi mpya utakuwa umefifisha ndoto zao.

Aidha, CPA Makalla amesema kuwa ingekuwa ni busara na bora wangesema washiriki uchaguzi na baada ya hapo wakae na kukubaliana ili kufanya mabadiliko.

“Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliposikia hoja hizi za kufanyika mabadiliko ya uchaguzi kutoka kwa wadau mbalimbali aliunda kikosi kazi kwa ajili ya kukusanya maoni na kutoa ushauri juu ya sheria zilizopo na akamteua Prof. Mkandara kuwa mwenyekiti wa kikosi hicho ili kuweza kufanya mabadiliko,” amesema Makalla.

Ameongeza kuwa, viliitwa vyama vyote kukutana na kutoa maoni na vyote vilishiriki isipokuwa Chadema kwani walisema walitaka kusikilizwa wakiwa peke yao na walimfata aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Abdulrahman Kinana.

spot_img

Latest articles

Papa mpya apatikana ni Robert Prevost

Na Mwandishi Wetu Papa Mpya wa Kanisa Katoliki Duniani, ametangazwa ni Kardinali Robert Francis Prevost(69),...

Waziri Masauni, Umoja wa Ulaya wajadili Mazingira

Mwandishi Maalum-Denmark Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad...

Serikali yasamehe faini za maji, yataka wananchi warejeshewe huduma

Na Mwandishi Wetu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ametangaza msamaha wa faini zote kwa wananchi...

Spika wa Bunge ateta na Dk. Mwapinga, amhakikishia ushirikiano

Na Mwandishi Wetu Spika wa Bunge la Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani...

More like this

Papa mpya apatikana ni Robert Prevost

Na Mwandishi Wetu Papa Mpya wa Kanisa Katoliki Duniani, ametangazwa ni Kardinali Robert Francis Prevost(69),...

Waziri Masauni, Umoja wa Ulaya wajadili Mazingira

Mwandishi Maalum-Denmark Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad...

Serikali yasamehe faini za maji, yataka wananchi warejeshewe huduma

Na Mwandishi Wetu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ametangaza msamaha wa faini zote kwa wananchi...