Aliyemuua mkewe na kumchoma na magunia ya mkaa, ahukumiwa kunyongwa

Na Mwandishi Wetu

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imemhukumu mfanyabiashara, Hamis Luwongo, kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mke wake, Naomi Marijani.

Uamuzi huo umetolewa leo Februari 26, 2025 na Jaji wa Mahakama hiyo, Hamidu Mwanga, baada ya kuridhishwa na ushahidi wa mashahidi 14 na vielelezo 10 uliotolewa mahakamani hapo.

Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo, jopo la mawakili wawili wa Serikali ukiongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali, Yasinta Peter akisaidiana na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Ashura Mnzava, uliomba Mahakama itoe adhabu kali dhidi yamshtakiwa huyo ili iwe fundisho kwa wanaume wote wanaowafanyia ukatili wanawake wao kwa kigezo wapo kwenye ndoa.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 44/2023, Hamis, mkazi wa Gezaulole, wilayani Kigamboni, alikuwa anakabiliwa na shtaka la mauaji ya mkewe Naomi Orest Marijani kinyume cha kifungu cha 196 na 197 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, kama ilivyorejewa mwaka 2019.

Anadaiwa kutenda kosa hilo Mei 15, 2019 nyumbani kwao kisha akauchoma mwili kwa kutumia magunia mawili ya mkaa ndani ya banda la kuku.

Inadaiwa masalia ya mwili na majivu alikwenda kuyazika shambani na kupanda migomba juu yake.

spot_img

Latest articles

Dk. Mwigulu: Tutamuenzi kwa vitendo marehemu Jenista

Na Mwandishi Wetu WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba amesema Serikali itayaendeleza mambo yote mema yaliyofanywa na...

Balozi Bandora kuzikwa kesho makaburi ya Kinondoni

Mwanadiplomasia nguli wa Tanzania, aliyewahi  kuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria na Mratibu Mkazi...

Serikali yajipanga kuimarisha utumishi wa umma, kuendeleza mageuzi ya kidigitali

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa...

Bokya amtahadharisha mapema Tyson wa Bongo

Na Winfrida Mtoi Bondia Ismail Khalid maarufu Boyka ametamba kutoa kipigo kikali kwa mpinza wake...

More like this