Zaidi ya watu 50 wafariki Congo kwa ugonjwa usiojulikana

Na Mwandishi Wetu 

ZAIDI ya watu 50 wamefariki Kaskazini Magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutokana na ugonjwa usiojulikana.

Mkurugenzi wa hospitali ya Bikoro, kituo cha ufuatiliaji wa afya, Serge Ngalebato, ameliambia shirika la habari la AP kwamba muda kati ya kuanza kwa dalili na kifo ni saa 48 kwa wagonjwa wengi.

Ngalebato amesema hali hiyo inatia wasiwasi na mlipuko wa ugonjwa huo usiojulikana ulitokea mnamo Januari 21 na hadi sasa wagonjwa 419 wameripotiwa, ikiwemo vifo vya watu 53.

Kwa mujibu wa ofisi ya WHO barani Afrika, mlipuko wa kwanza katika mji wa Boloko ulitokea baada ya watoto watatu kula popo na kufariki ndani ya saa 48 baada ya kuonyesha dalili za homa na kutokwa na damu.

Mwaka jana, ugonjwa mwengine usiojulikana ulisababisha vifo vya zaidi ya watu 100 kusini magharibi mwa Kongo japo baadaye iligundulika kuwa ni aina kali ya malaria.

Source: DW

spot_img

Latest articles

TCAA yaimarisha usalama wa anga kwa mifumo ya kisasa

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imejizatiti kuendana na mabadiliko...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ashiriki kikao cha wadau wa Mahakama

Na Mwandishi Wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza S. Johari ameshiriki katika kikao cha...

Waziri Ndejembi afungua kikao cha 55 cha Baraza Kuu la wafanyakazi wa Tanesco Dodoma

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi, leo tarehe 22 Januari, 2026 amefungua...

More like this