Watu watatu wafariki kwa ajali Kimara Stop Over

Na Mwandishi Wetu

WATU watatu wafariki na wengine wamejeruhiwa kwenye ajali iliyotokea usiku wa kuamkia Februari 14,2025 katika Mtaa wa Kimara Stop Over.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema ajali imehusisha lori lililohama njia na kuparamia kituo cha bodaboda kilichopo Kimara Stop Over.

Amesema Lori hilo lilikuwa likitokea Morogoro kuelekea Dar es Salaam na katika ajali hiyo hadi saa 9:00 alfajiri miili mitatu iliyokuwa imekandamizwa na kontena la lori hilo imeshatolewa.

“Miili ya watu hawa inasemekana walikuwa madereva pikipiki, pia tumefanikiwa kutoa pikipiki ambazo kwa idadi ni nyingi kuliko watu tuliowakuta kwa mantiki hiyo taarifa ya Polisi itaweka bayana,” amesema Chalamila.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, RPC Mtatiro Kitinkwi amesema kutokana na idadi ya pikipiki kuwa kubwa kuliko miili iliyokutwa, inawezekana wakati wa tukio watu walikimbia kujiokoa.

“Taarifa kwa kirefu tutaitoa tukishajua chanzo cha ajali hii kwa kuwa imetokea usiku na tumekuwa hapa kwa zaidi ya saa mbili,” amesema Kamanda Kitinkwi.

Baadhi ya mashuhuda wanasema gari hilo lilifeli brake na kukwepa daladala zilizokuwa zimebaki kwenye zebra na kuangukia watu waliokuwa wamesimama pembezoni mwa barabara pamoja na pikipiki 15, zilizokuwa zimeegeshwa kwenye eneo hilo.

spot_img

Latest articles

Rais Samia ashiriki Mkutano wa Dharura wa SADC kwa njia ya mtandao

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya...

Majaliwa azindua Kituo cha Mabasi Nzega Mjini

Na Mwandishi Wetu WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Machi 13, 2025 amezindua kituo kipya...

SEforALL kuimarisha ushirikiano upatikanaji nishati endelevu

📌 Dkt. Biteko asema Nishati Safi ya Kupikia ni ajenda endelevu 📌 Rais...

Umeme wa nje: Tutaepuka vipi vipigo vya nyuma?

Mwanzoni mwa wiki hii iliibuka habari kubwa iliyotokana na tamko la Rais wa Jamhuri...

More like this