Kesi ya DRC dhidi ya Rwanda kusikilizwa leo katika Mahakama ya haki za binadamu Arusha

Na Mwandishi Wetu

KESI iliyofunguliwa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) dhidi ya Rwanda katika Mahakama ya Afrika ya haki za watu na zile za Binadamu inasikilizwa leo jijini Arusha – huku Kongo ikiishitaki Rwanda kwa kukiuka mipaka ya kimamlaka ya Kongo, kuchochea machafuko mashariki kwa Kongo na kusababisha uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu.

Kesi hiyo itakayosikilizwa kwa siku mbili leo (12 Februari) na kesho (13 Februari) inahusu mapigano ya tangu Mwaka 2021, kati ya vikosi vya Kongo na waasi wa M23 ambao Kongo inadai wamekuwa wakifadhiliwa na Rwanda.

Kinshasa inadai kupitia mapigano hayo Rwanda na washirika wake wamesababisha watu zaidi ya 500,000 kukimbia makazi yao, huduma za kijamii kama hospitali na shule kufungwa na hata kusababisha watoto zaidi ya 20,000 kukosa elimu.

Madai mengine ya Kongo dhidi ya Rwanda yanahusu kuhifadhi wahalifu wa kivita bila ya kuwachukilia hatua za kisheria au kuwarudisha Kongo ili waadhibiwe kisheria.

Kwa kuileta kesi hiyo katika Mahakama hiyo ya kikanda, Kongo inatumaini mahakama hii itaitia hatiani Rwanda kwa ukiukwaji wa Mamlaka ya Mipaka ya Kiutawala ya Kongo, kuchochea machafuko na kusababisha uvunjifu mkubwa haki za binadamu.

Kwa madai hayo, Kongo inataka Mahakama iamuru Rwanda kuacha kufadhili vikundi vya waasi, kuondoa wanajeshi wake katika mipaka ya Kongo na kulipa fidia kwa waathirika wa machafuko yaliyosababishwa.

Rwanda inakanusha madai haya, na hata kutilia shaka mamlaka ya Mahakama kusikiliza kesi hiyo na inataka kesi itupiliwe mbali.

Source: BBC Swahili

spot_img

Latest articles

CHELSEA BINGWA WA FIFA CWC 2025

Timu ya Chelsea imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia la Klabu kwa kuchapa...

Humphrey Polepole ajiuzulu

Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya Ubalozi na...

Nandy ahamasika kutangaza Nembo ya Made in Tanzania Kimataifa

Na Tatu Mohamed MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Faustina Mfinanga (Nandy), amesema elimu aliyoipata...

Ndumbaro: Sheria 300 Zimetafsiriwa kwa Kiswahili Ili Kuimarisha Uelewa kwa Wananchi

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro, amesema kuwa hadi...

More like this

CHELSEA BINGWA WA FIFA CWC 2025

Timu ya Chelsea imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia la Klabu kwa kuchapa...

Humphrey Polepole ajiuzulu

Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya Ubalozi na...

Nandy ahamasika kutangaza Nembo ya Made in Tanzania Kimataifa

Na Tatu Mohamed MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Faustina Mfinanga (Nandy), amesema elimu aliyoipata...