Wahandisi nchini wametakiwa kufanyakazi kwa kuzingatia maadili

Na Mwandishi Wetu

WAHANDISI nchini wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, nidhamu na uwajibikaji kazini.

Wito huo umetolewa leo Februari 11, 2025 na Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), Mhandisi Bernard Kavishe wakati wa semina ya 18 ya utangulizi kwa wahandisi 362 waliojiandikisha katika Mpango wa Mafunzo kwa vitendo 362 waliojiandikisha mafunzo kwa vitendo (SEAP).

Amesema semina hiyo imelenga kuwajengea msingi imara watumishi wapya ili waweze kutimiza malengo ya Bodi kwa ufanisi.

“Mafunzo haya hua tunayatoa kila mwaka, ambapo tunawaelekeza wahandisi kufanya kazi kwa kuzingatia miiko na maadili yaliyowekwa na bodi,” amesema.

Aidha amesema na kutoa mafunzo hayo pia wahandisi zaidi ya 200 wameapa kiapo cha uadilifu.

“Kwa upande wa kiapo ambacho kimefanyika leo kinahusu moyo wa kujitoa na uadilifu, na kazi ya bodi ni kuwalea wahandisi tangu pale wanapomaliza shule mpaka wanapostaafu kuhakikisha wanaendelea kujinoa na kufanya kazi kuhakikisha mambo ya taifa hili yanaenda sawa,” amesema Kavishe.

Akifungua mafunzo hayo, Msajili wa bodi ya Wahandisi (ECI) kutoka nchini India, Dkt. Priya Swarup amesema kwa miaka mingi India na Tanzania wamekuwa wakishirikiana katika mambo mbalimbali.

“Sisi ni marafiki wa muda mrefu na tutaendelea kushirikiana katika mambo mbalimbali pamoja na kuwajengea uwezo katika masuala haya ya uhandisi,” amesema Swarup.

Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, Asha Mahimbo amesema semina hiyo itawasaidia kuwaongezea uzoefu na kujua soko lililopo nje linahitaji wahandisi wa aina gani.

“Lakini pia kuweza kuendana na sheria na taratibu za wahandisi ili mwisho wa siku tusije tukaonekana ni wahandisi ambao hatuendani na vigezo vya nchi husika,” amesema.

Aidha ametoa wito kwa wasichana kusoma masomo ya sayansi na kuacha kuyaogopa, Mhandisi Adrew Mongella ambaye ni miongoni wahandisi waliokula kiapo, amesema kiapo hicho kina maana ya kwamba unapokuwa mhandisi ni lazima uzingatie maadili yako na namna ya kuitumia taaluma yako kwaajili ya kujenga Taifa.

“Ni kiapo cha msingi kinaonesha utayari lakini pia kuzingatia maadili ya kitaaluma na sisi kama wahandisi tunao wajibu wa kujisimamia na kuzingatia miiko,” amesema Mongella.

spot_img

Latest articles

Waziri Aweso: Tuna uhakika wa maji ya kutosha Dar na Pwani

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amewatoa hofu wakazi wa mikoa ya...

PURA yajivunia mafanikio katika Ajenda ya Nishati Safi na ushiriki wa Watanzania Sekta ya Mafuta na Gesi

Na Tatu Mohamed MAMLAKA ya Kudhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imesema inajivunia...

Machungu, damu yamwagwa tena

Maadhimisho ya Saba Saba nchini Kenya ni tukio muhimu katika kukumbuka mapambano ya kudai...

eGA yatumia Sabasaba kuelimisha umma kuhusu Mfumo wa e-Mrejesho, yajivunia Tuzo ya Kimataifa

Na Tatu Mohamed MAMLAKA ya Serikali Mtandao (eGA) imeendelea kuonesha namna ambavyo Serikali inavyotekeleza mageuzi...

More like this

Waziri Aweso: Tuna uhakika wa maji ya kutosha Dar na Pwani

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amewatoa hofu wakazi wa mikoa ya...

PURA yajivunia mafanikio katika Ajenda ya Nishati Safi na ushiriki wa Watanzania Sekta ya Mafuta na Gesi

Na Tatu Mohamed MAMLAKA ya Kudhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imesema inajivunia...

Machungu, damu yamwagwa tena

Maadhimisho ya Saba Saba nchini Kenya ni tukio muhimu katika kukumbuka mapambano ya kudai...