Kilosa waanza kuonja Asali ya Hewa Ukaa

Na Mwandishi wetu, Morogoro

MKUU wa Wilaya ya KIlosa, Shaka Hamdu Shaka, amewataka wakazi wa wilaya hiyo kujikita katika biashara ya hewa ukaa, huo ndio ukombozi kwao kuanzia ngazi ya vijiji na halmashauri.

Akizungumza katika kikao cha kamati ya uvunaji misitu, Shaka amesema kwa sasa utajiri mkubwa upo katika biashara hiyo na kusema mfano umeonekana baada ya kazi kubwa iliyofanyika matokeo yake wameanza kuyaona.

Amesema waliingia katika majaribio na kuangaliwa kama wanaweza kufanya biashara hiyo wakapiga hatua, anaamini watakwenda kuwa mfano mzuri wa kusimamia rasilimali zilizopo katika wilaya hiyo.

“Ninaimani sana na ninyi kwamba mtakwenda kufanya mageuzi ya kulinda na kutunza rasilimali tulizonazo ili tija iweze kuonekana, lazima tukiri kwamba bado tunachangamoto, mfano mzuri ni migogoro kati ya kijiji na kijiji, kamati za maliasili za kijiji fulani kuvamia kijiji fulani.

“Watu wamezigeuza rasilimali kuwa mali ya watu binafsi, wanasimamia utunzaji misitu lakini wao wamekuwa ndio madalali wa kudalalia rasimali hizo ziweze kuuzwa kiholela,” amesema.

Shaka amevipongeza vijiji 10 ambavyo vilifanya vizuri kwamba wana faraja na kupata nguvu ya kuzungumza baada ya kuona namna jitihada zilivyozaa matunda kuanzia mwaka 2023 hadi Februari mwaka huu.

“Tunajivunia mafaniko haya kwa sababu tulidhamiria na kuhakikisha tunatekeleza maelezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kututaka kutumia vizuri fursa ya biashara ya hewa ukaaa kwa kutunza mazingira na misitu yetu ili tija ionekane, tunamshkuru kwa maono yake asali ya hewa ukaaa tumeanza kuionja Kilosa,” amefafanua Shaka.

Ameeleza kuwa, kwa mara ya kwanza Wilaya hiyo imeweza kuzalisha tani 545,433 ambazo ziitaingizia mapato ya sh. bilioni 1,171,478,458 ambapo ni gawio kulingana na mchanganuo wa mapato ambayo yamepatikana katika misitu ya vijiji huku kijiji Cha Malolo, msiba na Mhenda vikifanya vizuri zaidi katika kipindi cha 2023 mpaka Februari, 2024.

“Tunauwezo wa kupunguza umaskini kupitia bishara hii ya hewa ukaa, lakini pia tunauwezo wa kuifanya halmashauri hii kuwa ya mfano kupitia mapato haya ya biashara ya hewa ukaaa kadri uwekezaji huu utakavyozidi kutanuka” ameeleza.

Hata hivyo Shaka amepiga marufuku Uvunaji na usafishaji mashamba holela huku akisitiza kuchukuliwa kwa hatua kali za kisheria kwa wote wataobainika kufanya hivyo bila ya kuwa na vibali halali.

“Vijiji kwa kushirikiana na Halmashauri ya nendeni mkaboreshe sheria ndogo ndogo za usimamizi wa misitu ili kuweka adhabu kali zaidi kwa mtu yoyote atakayehusika na ukataji wa miti hovyo na uharibifu wa misitu” amesema Shaka.

spot_img

Latest articles

Baraza la saba la Wafanyakazi Wizara ya Nishati lakutana Dodoma

📌 Dkt. Kazungu asema Wizara itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya Kimkakati 📌 Baraza lapitisha rasimu...

Wizara ya Nishati yataja mafanikio utekelezaji majukumu 2024/25

📌 Uzalishaji umeme waongezeka kwa asilimia 59.9 📌 Misheni 300 kuongeza upatikanaji umeme...

Gavana Tutuba: Hali ya uchumi wa Tanzania inaendelea kuimarika

Na Tatu Mohamed GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba amesema kuwa, hali...

Dkt. Biteko: Ufundi Stadi umepewa kipaumbele na serikali

📌 Asisitiza kuwa, Rais Samia anajenga vyuo kila wilaya nchini 📌 Apongeza utoaji wa mafunzo...

More like this

Baraza la saba la Wafanyakazi Wizara ya Nishati lakutana Dodoma

📌 Dkt. Kazungu asema Wizara itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya Kimkakati 📌 Baraza lapitisha rasimu...

Wizara ya Nishati yataja mafanikio utekelezaji majukumu 2024/25

📌 Uzalishaji umeme waongezeka kwa asilimia 59.9 📌 Misheni 300 kuongeza upatikanaji umeme...

Gavana Tutuba: Hali ya uchumi wa Tanzania inaendelea kuimarika

Na Tatu Mohamed GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba amesema kuwa, hali...