Wataalam 2980 wajengewa uwezo kutoa huduma za afya ya akili

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Khamis Hamza Khamis amesema Serikali inaendelea kufanya jitihada mbalimbali za kudhibiti madhara ya mmomonyoko na kupanuka kwa kingo za mito.

Khamis amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Bagamoyo Muharami Mkengealiyetaka kujua ni lini Serikali itajenga Kingo za Mto Mpiji wilayani Bagamoyo mkoani Pwani zilizopanuka kutokana na Mvua kubwa na hivyo kuhatarisha nyumba za wananchi wa maeneo hayo.

Amesema jitihada zilizofanywa na Serikali ni pamoja na kuandaa Mwongozo wa Usafishaji wa Mito ili kuondoa mchanga na tope ambapo kikosi kazi kimeundwa kwa ajili ya kushughulikia suala la usafishaji wa mito.

“Mheshimiwa Naibu Spika, Sheria ya Mazingira sura 191 kifungu cha 57 (2) kimempa Waziri mamlaka ya kutunga kanuni ndogo na mwongozo na tayari kuna hatua zimeanza kuchukuliwa kwa kufanya doria na kuzuia mali au gari litakalokutwa na kupigwa faini,” amesema Khamis.

Pamoja na hatua hiyo, Naibu Waziri Khamis ameongeza kuwa Serikali inaendelea kutoa elimu kwa wananchi ili watambue umuhimu wa kutunza mazingira katika mito.

Aidha, ameeleza kuwa katika kudhibiti athari za mvua, Serikali inatumia njia za asili za kudhibiti mmomonyoko wa kingo za mito kwa kupanda miche 5,000 aina ya michikichi, migomba, miti maji na matete katika kingo za mto katika eneo lenye ukubwa wa ekari 100 katika Kata ya Mabwepande wilayani Kinondoni mkoani Dar e Salaam.

spot_img

Latest articles

Taasisi za Umma Kukabidhi gawio Ikulu Juni 30 Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina imetangaza siku ya Gawio 2026 itafanyika...

DC Mbarali aongoza zoezi la upandaji miti kuhifadhi mazingira ya mradi wa TAZA

📌 Lengo ni kuimarisha na kuhifadhi mazingira 📌 Maeneo yenye vyanzo vya maji vinavyochangia uzalishaji...

Wachezaji volleyball nchini watakiwa kujituma kuwavutia mawakala wa kimataifa

Na Mwandishi Wetu WACHEZAJI wa mpira wa wavu 'volleyball' wanaoshiriki Ligi ya Mkoa wa Dar...

More like this

Taasisi za Umma Kukabidhi gawio Ikulu Juni 30 Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina imetangaza siku ya Gawio 2026 itafanyika...

DC Mbarali aongoza zoezi la upandaji miti kuhifadhi mazingira ya mradi wa TAZA

📌 Lengo ni kuimarisha na kuhifadhi mazingira 📌 Maeneo yenye vyanzo vya maji vinavyochangia uzalishaji...