Uzinduzi wa biashara saa 24 Dar kufanyika Februari 22, 2025

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

UZINDUZI wa biashara saa 24 jijini Dar es Salaam unatarajiwa kufanyika Februari 22, mwaka huu.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila katika mkutano wake na waandishi wa habari.

Amesema uzinduzi huo utaanzia eneo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa hadi Kariakoo na kutakuwa na matukio tofauti tofauti katika maeneo mbalimbali yatakayopangwa.

Chalamila amefafanua kuwa, ufanyaji biashara kwa saa 24 unalenga kuimarisha uchumi wa Mkoa, kuongeza mapato ya serikali.

“Maandalizi ya ufungaji wa kamera za CCTV na taa za barabarani yanaendelea ili kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unadumishwa.

“Tutahakikisha mkoa wetu wa Dar es Salaam unakuwa na mazingira bora ya kufanya biashara muda wote, na tayari tunashirikiana na viongozi wa halmashauri kuimarisha maeneo yanayofaa kwa biashara za masaa 24,” amesema Chalamila.

Aidha ameongeza kuwa mpango huo utaimarisha uchumi na kuwanufaisha wafanyabiashara na wakazi wa jiji hilo.

Ameongeza kuwa, mji huo lazima ujengwe kwa kiwango cha kimataifa hivyo amebainisha kuwa tayari kamati imeshaundwa ya kukagua na kupitia majengo chakavu ambayo wanaoyamiliki wataombwa kuingia ubia na walio na uwezo kuyaendeleza ili kusaidia kutokuwepo kwa majengo yasiyo na hadhi ya kukaa katika ya mji.

Akizungumzia suala la ujenzi wa soko la Kariakoo Chalamila amesema zaidi ya Sh. Bilioni 28 zimetolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya ujenzi wa soko hilo na kwamba ujenzi wake umefikia asilimia 97 pia amesema kwa sasa bodaboda na bajaji hazijazuiliwa kuingia katikati ya jiji kwani walizuiwa kwa siku chache kutokana na ugeni wa marais wa Afrika.

Kuhusu Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wa Nishati uliofanyika Januari 27 hadi 28 Mwaka huu jijini Dar es Salama, RC Chalamila amewashukuru na kuwapongeza wananchi wa mkoa huo kwa ushirikiano mkubwa walioutoa ikiwemo kuimarisha amani, utulivu na usafi hivvyo ameelekeza wilaya zote kuendelea kusimamia suala la usafi ili Mkoa uendelee kuwa kivutio huku akisisitiza kuwa Serikali inakusudia kuanza kutumia usafiri wa treni na majini kuimarisha usafiri ndani ya jiji hilo.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Soko la Kariakoo Hawa Ghasia amesema kuanzia Januari 31, mwaka huu wanaanza kuweka majina ya wafanyabiashara ambao walikuwepo kwenye soko la Kariakoo kabla halijaungua ili wasajiliwe na kwamba baada ya hapo watasajili wafanyabiashara wapya na waliokuwa wanadaiwa wanapaswa kulipa madeni yao.

“Januari 31, mwaka huu ndo tunaanza zoezi la kuweka majina ya waliokuwa wakifanya biashara lakini kwa masharti, mtu anayejua anadeni la nyuma alipe kwanza deni lote kwani hawaruhusu.

“Baada ya hapo ndo tutangaza fursa kwa Wafanyabiashara wapya, ambapo wataomba nafasi kupitia mfumo wa Tausi…asidanganye mtu kuwa atoe hela ndo apate nafasi, kuna mfumo wa kuomba maombi hayo na tukishauruhusu ufanye kazi tutawatangazia,” amesisisitiza Hawa.

spot_img

Latest articles

MINZIRO NA PAMBA YAKE NAWAPIGA TU

Na Mwandishi Wetu Timu ya Pamba Jiji chini ya Kocha Felix Minziro (Majeshi, Baba Isaya)...

Majaliwa azitaka Mamlaka za Mikoa, Taasisi za Elimu kusimamia utekelezaji Sera ya elimu

Na Mwandishi Wetu WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amezielekeza mamlaka za mikoa, halmashauri na taasisi za...

Bidhaa ‘feki’ zadidimiza Watanzania lindi la umasikini

Watanzania wanazidi kunasa katika mzunguko wa umasikini unaosababishwa na kushamiri kwa bidhaa duni na...

More like this

MINZIRO NA PAMBA YAKE NAWAPIGA TU

Na Mwandishi Wetu Timu ya Pamba Jiji chini ya Kocha Felix Minziro (Majeshi, Baba Isaya)...

Majaliwa azitaka Mamlaka za Mikoa, Taasisi za Elimu kusimamia utekelezaji Sera ya elimu

Na Mwandishi Wetu WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amezielekeza mamlaka za mikoa, halmashauri na taasisi za...