TANZANIA NA SOMALIA KUBADILISHANA WAFUNGWA

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

SERIKALI ya Tanzania na Somalia zimesaini mikataba miwili ya makubaliano ya kushirikiana katika masuala ya ulinzi na usalama na kubadilishana wafungwa.

Mikataba hiyo imesainiwa leo Januari 29, 2025 jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa kwa upande wa Tanzania na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Ahmed Moalim Fiqi kwa upande wa Somalia.

Akizungumza baada ya kusaini mikataba hiyo, Bashungwa amesema mkataba wa kubadilishana wafungwa utaziwezesha nchi hizo mbili kuruhusu wafungwa waweze kutumikia adhabu katika nchi zao na kusaidia kupunguza gharama za kifedha za kuwahudumia wafungwa hao.

“Inapotokea kuna Watanzania wenzetu wameingia katika hali ya kuwa wafungwa wakiwa kule Somalia, kupitia mkataba tuliosaini utatuwezesha kuwachukuwa Watanzania kuwaleta kwenye magereza yetu, vile vile kwa wafungwa wa Somalia watarudishwa kuendelea na vifungo vyao nchini kwao,” ameeleza.

Aidha, Bashungwa amesema mkataba wa ushirikiano kuhusu ulinzi na usalama, unalenga kuimarisha uwezo vyombo vya usalama kwa kutoa mafunzo kwa Askari wa pande zote mbili, kutekeleza operesheni za pamoja, kubadilishana utaalam katika masuala ya usalama na ulinzi pamoja na kubadilishana taarifa za kiintelijensia.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Mussa amesema utiaji saini wa mikataba hiyo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Shirikisho ya Somali, Hassan Sheikh Mohamud ili kuendelea kuimarisha ushirikiano.

spot_img

Latest articles

MINZIRO NA PAMBA YAKE NAWAPIGA TU

Na Mwandishi Wetu Timu ya Pamba Jiji chini ya Kocha Felix Minziro (Majeshi, Baba Isaya)...

Majaliwa azitaka Mamlaka za Mikoa, Taasisi za Elimu kusimamia utekelezaji Sera ya elimu

Na Mwandishi Wetu WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amezielekeza mamlaka za mikoa, halmashauri na taasisi za...

Bidhaa ‘feki’ zadidimiza Watanzania lindi la umasikini

Watanzania wanazidi kunasa katika mzunguko wa umasikini unaosababishwa na kushamiri kwa bidhaa duni na...

More like this

MINZIRO NA PAMBA YAKE NAWAPIGA TU

Na Mwandishi Wetu Timu ya Pamba Jiji chini ya Kocha Felix Minziro (Majeshi, Baba Isaya)...

Majaliwa azitaka Mamlaka za Mikoa, Taasisi za Elimu kusimamia utekelezaji Sera ya elimu

Na Mwandishi Wetu WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amezielekeza mamlaka za mikoa, halmashauri na taasisi za...