FEZA SCHOOLS YAJIVUNIA UWEKEZAJI, KUTOA WANAFUNZI BORA

Na Mwandishi Wetu

Baada ya kufaulisha wanafunzi wote katika mtuhani wa kidato cha nne, Shule Feza Boys imejivunia uwekezaji iliyofanya katika kumuandaa mwanafunzi bora, ikiutaja kuwa ndio siri ya kufanya vizuri kila mwaka.

Hayo ameyasema Makamu Mkuu wa Shule ya Feza Boys, Shabani Mbonde wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 23,2025 katika shule hiyo iliyopo Kunduchi Dar es Salaam mara baada ya Baraza la Mitihani Tanzania kutangaza matokeo ya kidato cha nne.

Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Feza Boys wakishangilia kwa kumbeba mwanafunzi mwenzao,Moses Mwaijande aliyefanya viziuri katika matokeo ya kidato cha nne kwa kupata ufaulu wa alama A kwa masomo yote (1.7)jumla ya wanafuzi wote katika shule hiyo wamepata ufaulu wa alama A.

Mbone ameleeza kuwa matokeo hayo ambapo asilimia zaidi ya 65 ya wanafunzi wao wamefaulu katika daraja la kwanza kwa 1.7, hajatokea kirahisi bali imechangiwanna uwekezaji na mazingira ikiwamo walimu wa kutosha.

” Feza Schools haitoi mwanafunzi bora katika A tu, bali katika nyanja zote.Sisi katika elimu hatumjengi mwanafunzi kupata A tu lakini pia katika kukabiliana na hali zote katika maisha kulingana na wakati uliopo.

“Hii yote inatokana na jitihada mbalimbali za wanafunzi wenyewe na walimu. Mwanafunzi wetu anakuwa ni kama ametoka kwenye mashine au kiwanda kilichomjenga katika kupambana na changamoto mbalimbali katika mtihani na maisha.Tunajivunia wanafunzi wetu na walimu wetu,” amesema Makamu Mkuu huyo.

Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Feza Boys wakishangilia kwa kumbeba mwanafunzi mwenzao,Allan Masaka aliyefanya viziri katika matokeo ya kidato cha nne kwa kupata ufaulu wa daraja 1.7 jumla ya wanafuzi wote katika shule hiyo wamepata ufaulu wa alama A.

Aidha Mbonde amesema kama sekta binafsi wanashukuru serikali kwa kusisitiza suala la elimu na wanaiunga mkono Serikali katika kuhakikisha elimu inakuwa bora.

Naye Mkuu wa taaluma msaidizi wankidato cha tatu na nne, Abdallah Juma ameeleza mbinu wanazotumia kuwafundisha wanafunzi hao kuwa ni progamu mbalimbali walizonazo shuleni hapo.

” Sio kwamba sisi vijana wote tunaowachukua ni wale ‘cream’ tu bali wanakuja hata wenye uwezo mdogo tunawatengeneza na wanakiwa sawa na wenzao na wanafaulu kwa pamoja.

” Matokeo haya yamepatikana kwa njia tofauti, pande zote tatu zina mchango yaani wazazi, walimu na wanafunzi, pia tuna programu mbalimbali za masomo kuanzia asubuhi, jioni na hata usiku, pia wanapata muda wa kucheza”, amesema.

Kwa upande mmoja wa wanafunzi wa FEZA BOYS waliofanya vizuri kwa kupata division one 1.7, Moses Francis, amesema anamshukuru Mungu kwani mafanikio hayo hayakuja kirahisi ya kupata A masomo yote 10 ila mazingira ya shule yamechangia ikiwamo kusoma kwa bidii kama mwanafunzi.

Amefafanua kuwa kutokana na ratiba za shule zilivyopangiliwa wanapata muda wa kutosha wa kupumzika lakini kuna kipindi kigumu unatakiwa kusoma sana ili kufaulu mtihani.

“Hii haipatikani kirahisi, mtu kufaulu lazima kuwe na motisha kuanzia kwa mwanafunzi wenyewe na mzingira mazuri ya kujifunzia pamoja na kumtanguliza Mungu.Kila wiki tunafanya mazoezi ya masomo kwa kufanya test,” amesema Moses.

Katika matokeo ya kidato cha nne yaliyotangazwa leo na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), ufaulu umeongezeka ambapo jumla ya watahiniwa wa shule 477,262 kati ya 516,695 wenye matokeo sawa na asilimia 92.32 wamefaulu kwa kupata madaraja ya I,II,III,IV.

spot_img

Latest articles

TANESCO YABORESHA MAISHA YA WAFANYAKAZI NYUMBA YA MUNGU

📌 Nyumba za wafanyakazi zakarabatiwa, kuboresha utendaji wa kazi 📌 Mtambo wa kisasa wa kuchakata...

KATAMBI ATOA ONYO KWA MAKUNDI YA ULINZI YASIYO RASMI

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, ametoa onyo kwa...

Watumishi OTR wapatiwa mafunzo ya Mfumo wa Usimamizi wa Ubora

Na Mwandishi wa OTR OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) imeendelea na hatua za kuimarisha...

MRADI WA UMEME MPOMVU – GGM KUIMARISHA UPATIKANAJI WA UMEME NA KUCHOCHEA SHUGHULI ZA KIUCHUMI GEITA – MHE. SALOME

📌 Kukamilika kwa njia mpya kutatoa fursa kwa njia ya awali kuendelea kunufaisha wananchi...

More like this

TANESCO YABORESHA MAISHA YA WAFANYAKAZI NYUMBA YA MUNGU

📌 Nyumba za wafanyakazi zakarabatiwa, kuboresha utendaji wa kazi 📌 Mtambo wa kisasa wa kuchakata...

KATAMBI ATOA ONYO KWA MAKUNDI YA ULINZI YASIYO RASMI

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, ametoa onyo kwa...

Watumishi OTR wapatiwa mafunzo ya Mfumo wa Usimamizi wa Ubora

Na Mwandishi wa OTR OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) imeendelea na hatua za kuimarisha...