EL NIÑO YABADILI RATIBA YA MITIHANI 2026

Na Mwandishi Wet

Tishio la mvua kubwa zinazohusishwa na hali ya hewa ya El Niño limeifanya Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kubadili ratiba ya baadhi ya Upimaji na Mitihani ya Taifa ya mwaka 2026, kwa lengo la kuhakikisha usalama wa watahiniwa na uendeshaji mzuri wa mitihani.

Akizungumza Septemba 25, jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wanu Hafidh Ameir, amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua kuhakikisha hali ya hewa haiathiri uendeshaji wa mitihani na usalama wa wanafunzi.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, Mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Pili utaanza Oktoba 12 na kukamilika Novemba 6, 2026, huku Mtihani wa Kidato cha Nne ukianza Oktoba 19 na kumalizika Novemba 6, mwaka huu.

Aidha, Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne utafanyika Oktoba 6, wakati Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Pili ngazi ya shule utafanyika Oktoba 7 na 8, mwaka huu.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Prof. Said Mohammed, amesema kamati za mitihani zinapaswa kufanya maandalizi ya kutosha, ikiwamo kuhakikisha vituo vina mazingira salama na watahiniwa wanafika kwa wakati.

Amewataka wakuu wa shule kuwafahamisha watahiniwa kuhusu ratiba hiyo na mabadiliko yaliyofanyika, huku wazazi na walezi wakitakiwa kuhakikisha wanafunzi, hasa wa shule za kutwa, wanafika katika vituo vya mitihani kwa wakati.

Amesema Serikali na NECTA zitaendelea kutoa maelekezo kulingana na mwenendo wa hali ya hewa, hususan kadiri kipindi cha mitihani kinavyokaribia.

Amesisitiza kuwa kila mwanafunzi mwenye sifa anapaswa kupata haki ya kufanya mtihani, huku kamati za mitihani zikitakiwa kutambua mapema changamoto zinazoweza kuathiri usafiri na ufikaji wa watahiniwa katika vituo vya mitihani.

Ratiba na maelekezo ya mitihani yamewekwa katika tovuti rasmi ya NECTA, huku shule zikitakiwa kuhakikisha taarifa hizo zinawafikia watahiniwa na wazazi kwa wakati.

spot_img

Latest articles

TUME YATANGAZA RATIBA YA UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE CHAMWINO NA UDIWANI KATA 11

Na Mwandishi Wetu Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza Novemba 04, 2026 kuwa...

MKOA WA RUKWA MBIONI KUUNGANISHWA KWENYE GRIDI YA UMEME YA TAIFA

Na Mwandishi Wetu, Iringa Wananchi wa Mkoa wa Rukwa wanatarajiwa kuanza kunufaika na huduma ya...

Akwilapo: Teknolojia mpya muhimu kukabiliana na mahitaji ya ujenzi

Na Mwandishi Wetu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Leonard Akwilapo, ametoa wito...

FILAMU YA ‘THE RHINO OF NGORONGORO’ YAZINDULIWA

Na Mwandishi Wetu, Ngorongoro KATIKA kuadhimisha Siku ya Faru Duniani, inayoadhimishwa Septemba 22 kila mwaka,...

More like this