Media Brains, KAS zawajengea uwezo waandishi kutambua habari feki, washiriki   wafunguka walivyonufaika na mafunzo

Na Winfrida Mtoi

Kampuni ya Media Brains ikishirikiana na Shirika la Konrad Adenauer Stiftung (KAS) wameendesha mafunzo ya kuwajengekea uwezo waandishi wa habari katika kukabiliana na habari za uongo (fake news).

Mafunzo hayo yanayofadhiliwa na KAS ni muendelezo wa programu ya kuwajengea uwezo waandishi wa Tanzania kumudu uandishi wa habari wa kidijitali na kuzitambua habari za kughushi, hasa katika zama hizi za ambazo kasi ya matumizi ya majukwaa ya kidigitali kusambaza taarifa za uongozo ikiwa kubwa.

Katika mafunzo yaliyofanyika kwa siku tatu jijini Dar es Salaam wiki hii, wawezeshaji ni waandishi waandamizi Absalom Kibanda na Jesse Kwayu, wote kutoka Kampuni ya Media Brains.

Mkurugenzi wa Mtendaji wa Media Brains, Jesse Kwayu

Wakiwanoa waandishi hao, wawezeshaji walifundisha baadhi ya mbinu za kiteknolojia na mifumo kama vile Akili Unde (Altificial Intellgence (AI), zinatumika kusambaza habari potofu na njia za kutumia ili kuzitambua taarifa za uongo.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Mtendaji wa Media Brains, Jesse Kwayu, ameeleza ni muhimu kwa waandishi wa habari kuzidi kuongeza ujuzi ili kukabiliana na taarifa za uongo ambazo zimekuwa ni tatizo kwa sasa.

“Katika ulimwengu huu wa maendeleo ya sayansi na teknolojia, katika ulimwengu  wa kidigitali, kunakuwa  na mambo ya kuleta taarifa potofu, uzushi, uongo kwa hiyo zinaathiri. Ni lazima waandishi wa habari wafahamu habari ghushi zinaanzia wapi, zinaishia wapi,”

Ofisa Operesheni Mkuu wa Media Brains, Absalom Kibanda

Ameeleza kuwa habari potofu zimekuwa zikiathiri ustawi wa jamii kiuchumi, kisaikolojia na namna mbalimbali, hivyo mafunzo hayo yatasaidia wanahabari kupunguza usambaaji wa taarifa za kughushi.

Naye Ofisa Operesheni Mkuu wa Media Brains, Absalom Kibanda, amewakumbusha waandishi kuwa upotoshaji wa taarifa haupo Tanzania pekee bali dunia nzima inakabiliana na majaribu ya kidigitali yanayohusisha habari za uongo.

“Ili kurudisha imani kwa walaji wa habari, tunajaribu kutoa mafunzo ya kuwafanya  waandishi kuhakiki kila habari  unayoposti katika mtandao, kujua  ukweli wake kabla hujawalisha walaji,” amesisitiza Kibanda.

Mkurugenzi Mkaazi wa KAS, Peter Koch

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkaazi wa KAS, Peter Koch ambao ni wafadhili wa mafunzo hayo, amesema lengo ni kuwapa washiriki nafasi ya kufanya mafunzo ya vitendo badala ya kusikiliza pekee, hivyo mwakani wana mipango ya kuendeleza warsha hizo kwa kugusia mada nyingine muhimu.

“Kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na nyenzo na mbinu za kuweza kutambua  na kuchuja taarifa za uongo katika vyanzo mbalimbali za video na taarifa katika maisha na  kazi za kila siku,” amesisiza Koch.

Baadhi ya waandishi walioshiriki mafunzo hayo, walieleza jinsi alivyonufaika na kuongeza uelewa wa matumizi ya zana mbalimbali za kiteknolojia katika kutambua taarifa za uzushi na uongo.

“Katika siku hizi tatu, Media Brains na KAS wamenisadia kutoka katika uelewa mdogo na kuwa na uelewa mkubwa wa kuandika habari nzuri na kukweba habari za uongo,” amesema Zubeda Kinyanguli mwandishi kutoka Mkoa wa Geita.

Naye Nickson Mwageni amesema kuwa:“Tumejifunza vitu vingi, nimejifunza kuwa nikipata stori yoyote nisiharakishe kuposti, ninatakiwa kufanya uhakiki kwa pande zote mbili. Pia tumejifunza tools za kuhakiki picha na video, zitatusaidia hususani sisi wa digital.

“Tunawapongeza wenzetu hawa wa KAS na Media Brains, kupitia mafunzo haya bila shaka kila alikuja hapa amenufaika, tuendelee kuomba Mungu ili tuweze kunufaika zaidi,”

Programu ya mafunzo ya uandishi wa habari wa kidigitali zinazoendeshwa kwa ushirikiano wa taasisi hizi mbili, tayari imefanyika katika mikoa ya Manyara, Arusha, Singida, Dodoma, Iringa, Kagera.

spot_img

Latest articles

EL NIÑO YABADILI RATIBA YA MITIHANI 2026

Na Mwandishi Wet Tishio la mvua kubwa zinazohusishwa na hali ya hewa ya El...

TUME YATANGAZA RATIBA YA UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE CHAMWINO NA UDIWANI KATA 11

Na Mwandishi Wetu Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza Novemba 04, 2026 kuwa...

MKOA WA RUKWA MBIONI KUUNGANISHWA KWENYE GRIDI YA UMEME YA TAIFA

Na Mwandishi Wetu, Iringa Wananchi wa Mkoa wa Rukwa wanatarajiwa kuanza kunufaika na huduma ya...

Akwilapo: Teknolojia mpya muhimu kukabiliana na mahitaji ya ujenzi

Na Mwandishi Wetu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Leonard Akwilapo, ametoa wito...

More like this

EL NIÑO YABADILI RATIBA YA MITIHANI 2026

Na Mwandishi Wet Tishio la mvua kubwa zinazohusishwa na hali ya hewa ya El...

TUME YATANGAZA RATIBA YA UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE CHAMWINO NA UDIWANI KATA 11

Na Mwandishi Wetu Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza Novemba 04, 2026 kuwa...

MKOA WA RUKWA MBIONI KUUNGANISHWA KWENYE GRIDI YA UMEME YA TAIFA

Na Mwandishi Wetu, Iringa Wananchi wa Mkoa wa Rukwa wanatarajiwa kuanza kunufaika na huduma ya...