Na Winfrida Mtoi
Yanga imemtangaza kocha Sead Ramovic raia wa Ujerumani kuchukua nafasi ya Miguel Gamond.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 45, alikuwa akikinoa kikosi cha Ts Galaxy ya Afrika Kusini tangu mwaka 2021-2024.
Kabla ya kumtangaza kocha huyo Yanga ilitoa taarifa leo Novemba 15, 2024 kuwa imevunja mkataba na Gamondi pamoja na msaidizi wake Moussa Ndaw.