Waziri Mkuu ateta na Mwenyekiti wa Bodi ya CITIBANK

Na Mwandishi Maalum

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imekuwa inafanya kazi na benki ya Citibank ya Marekani kwa zaidi ya miaka 35 na imekuwa ikipokea ushauri wa mambo ya kifedha kupitia Benki Kuu ya Tanznaia (BoT).

Amesema hayo jana Septemba 24, 2024 alipokutana na Mwenyekiti wa Citibank,  John Dugan, kwenye makao makuu ya benki hiyo, jijini New York, Marekani.

“Serikali ya Tanzania inaishukuru sana Benki ya Citibank kwa kuwa imeshiriki katika ujenzi wa uchumi ikiwemo na upatikanaji wa fedha za mikopo, kuishauri Serikali katik amasuala ya fedha na kufadhili miradi mikubwa inayoendelea kujengwa nchini,”

“Benki hii imekuwa ikikopesha makampuni yanayojenga reli yetu ya SGR na ili kuhakikisha wanachangia ujenzi wa uchumi wa Tanzania, na wao pia wamechukua lot moja ya ujenzi wa reli hiyo na kufadhili ujenzi wake. Hali kadhalika uendelezaji wa uwanja wa ndege wa Pemba,” amesema.

Ameeleza kuwa Tanzania ilipokabiliwa na uhaba wa mafuta ya kuendeshea mitambo na magari, hivyo benki hiyo ilitumika kuwasaidia wafanyabiashara kupata mafuta kwa bei nafuu.

Mbali na ushauri wa masuala ya kiuchumi, Waziri Mkuu amesema benki hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Maendeleo ya Marekani, (U.S. International Development Finance Corporation) pia ilitoa mikopo kwa wafanyabiashara wadogo huku ikiwapatia fursa zaidi akina mama na wasichana wanaomiliki biashara zao binafsi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Citibank  Marekani, Dugan amesema wataendelea kushirikiana na Serikali katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo kama walivyofanya katika miaka 40 iliyopita.

spot_img

Latest articles

NIRC kutekeleza miradi 30 ya umwagiliaji, kufungua maelfu ya ajira kwa vijana

Na Mwandishi Wetu, Dodoma SERIKALI kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) imezindua mkakati wa...

TTB yampokea Mr. Alaya anayewania Guinness World Records

Na Mwandishi Wetu TANZANIA imepokea mhamasishaji amani duniani, Saddam Alaya (Mr. Alaya), ambaye anatekeleza...

VETA yaleta suluhisho la kupiga mpunga kwa wakulima

Na Mwandishi Wetu, Dodoma MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imekuja na...

TAMKU yatanua uwekezaji, kujenga kiwanda cha korosho Tunduru

Na Mwandishi Wetu CHAMA Kikuu cha Ushirika cha TAMKU kimeanza kutekeleza mkakati wa kupanua...

More like this