Tanzania, Morocco katika jukwaa la biashara

NA GRACE MWAKALINGA

SERIKALI ya Morocco imeandaa Jukwaa la Biashara na Tanzania kwa lengo la kujenga na kukuza ushirikiano wa biashara, pamoja na kufungua fursa katika sekta za kilimo, utalii, miundombinu, nishati mbadala, usimamizi wa bandari na teknolojia.

Balozi wa Ufalme wa Morocco nchini, Zakaria El Goumiri amesema ushirikiano wa nchi hizo mbili ukuza biashara baina ya nchi hizo mbili na kwamba takwimu zinaonesha ukuaji kutoka dola milioni 28 mwaka 2016 hadi dola milioni 285.5 mwaka 2022.

Balozi El Goumiri alikuwa akizungumza kwenye hafla ya maadhimisho ya miaka 25 tangu kutawazwa Mfalme Mohammed wa VI wa Morocco.

“Serikali zetu zimekubaliana kuandaa awamu ya pili ya Jukwaa la Biashara la Morocco na Tanzania baadaye mwaka huu, dhumuni litakuwa ni kubaini fursa mpya za uwekezaji, kujenga ushirikiano thabiti, na kuendeleza maendeleo ya nchi zetu mbili,” El Goumiri.

Kwa upande wake Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Pindi Chana amesema maadhimisho ya Miaka 25 ya kuwekwa Madarakani kwa Mtukufu Mfalme Mohammed VI ni fursa nzuri ya kutafakari juu ya mafanikio ambayo Ufalme wa Morocco umeyapata tangu tarehe Julai 30, 1999.

Dk. Chana anasema Ufalme huo umekuwa ukitoa misaada ambayo inajumuisha utoaji wa zaidi ya nafasi za masomo 8,000 kwa nchi kadhaa za Afrika, ikiwemo Tanzania.

“Tanzania na Morocco zina uhusiano wa muda mrefu ambao ulianza hata kabla ya ukoloni ambapo watu wetu walikuwa wakishirikiana kwa karibu kupitia biashara na shughuli nyingine za kijamii na kitamaduni,” anasema Waziri Chana na kuongeza:

“Ushirikiano umezidi kuimarika baada ya ziara ya Kiserikali ya Mtukufu Mfalme nchini Tanzania mnamo Oktoba 2016 na wakati wa ziara hiyo, mikataba 22 ilisainiwa katika maeneo mbalimbali ya ushirikiano, ikiwa ni pamoja na ulinzi na usalama, biashara na uwekezaji, kilimo, utalii, usafiri, afya, elimu, utamaduni, na michezo,” amesema Dk. Balozi Pindi Chana.

spot_img

Latest articles

Tulia alipoteza fursa ya kuokolewa uhai wa Kibao

INAWEZEKANA Agosti 27 2024 ilikuwa ni siku ambayo maisha ya Ally Mohamed Kibao yangeokolewa...

DCEA yakamata kilo 1,815 za skanka

Na Mwandishi Wetu Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imewakamata...

Waziri Mkuu: Suala la mazingira liwe ajenda ya Kitaifa

Na Mwandishi Wetu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema suala la uhifadhi wa mazingira liwe...

NECTA yawaonya wamiliki na wakuu wa shule

Na Winfrida Mtoi Baraza la Mtihani la Tanzania (NECTA), limewataka wamiliki na wakuu wa shule...

More like this

Tulia alipoteza fursa ya kuokolewa uhai wa Kibao

INAWEZEKANA Agosti 27 2024 ilikuwa ni siku ambayo maisha ya Ally Mohamed Kibao yangeokolewa...

DCEA yakamata kilo 1,815 za skanka

Na Mwandishi Wetu Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imewakamata...

Waziri Mkuu: Suala la mazingira liwe ajenda ya Kitaifa

Na Mwandishi Wetu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema suala la uhifadhi wa mazingira liwe...