Wadau washauri Mjadala wa Kitaifa Kuhusu Haki za Binadamu na Uhifadhi

Na Mwandishi Wetu, Media Brains

Wadau wa kutetea haki za binadamu na utawala bora wamependekeza kufanyika kwa mjadala wa kitaifa kuhusu haki za binadamu na uhifadhi, wakiamini hatua hiyo itaondoa athari zilizopo sasa, ikiwemo ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

Hayo yamebainishwa Juni 28, 2024, jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Center for Strategic Litigation, Deus Valentine, wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Tuhifadhi Uhai: Ukiukwaji wa Haki za Binadamu Sekta ya Hifadhi Tanzania. Ripoti hiyo imeangazia athari mbalimbali zinazowakumba wananchi wanaozungukwa na hifadhi nchini.

Deus amesema kuwa kadri sekta ya utalii inavyozidi kukua nchini, malalamiko na vilio kuhusu haki za binadamu na haki nyingine zinazohusiana na uhifadhi zimeendelea kuibuka.

“Ingawa sekta ya utalii ni muhimu na imeendelea kuchangia mapato makubwa zaidi ya Dola bilioni 3.6 kwa mwaka, ni sekta muhimu sana ambayo tunatakiwa kulinda na kuikuza kwa ustawi wa taifa letu. Lakini tunapoendelea kuilinda na kuikumbatia sekta hii, ni vema kutambua haki za wale wanaotusaidia kuilinda.

“Tunahitaji mjadala wa kitaifa ili kufanya jamii zinazosaidia uhifadhi kuwa sehemu ya mipango hii, kwani kila mmoja anaathiriwa na shughuli za uhifadhi. Swali ni namna gani tunatambua haki za wahifadhi wa asili; suluhu yake ni kuwa na mjadala wa kitaifa ili kufanya jamii zinazosaidia uhifadhi kuwa sehemu ya mipango hii,” amesema Deus.

Deus ameongeza kuwa, mipango mingi ya maendeleo inatengenezwa kana kwamba jamii zinazozunguka sekta ya uhifadhi siyo sehemu ya sekta yenyewe.

“Licha ya ukweli kuwa kabla ya serikali kuja na kuanzisha utaratibu wa kusimamia hifadhi, maeneo haya yalikuwa yakisimamiwa na wananchi wenyewe kama wahifadhi wa asili,” amesema Deus.

Amesema iwapo tutatambua uwepo na nafasi ya pekee ya jamii zinazozunguka hifadhi zetu, itakuwa rahisi kuondoa malalamiko mengi ambayo yamebebwa na ripoti hiyo.

“Mwaka 2007 tulianzisha sera ya Local Content Policy ikiwa na maana kwamba uwekezaji mkubwa unaokuja nchini unakuwa na manufaa kwa jamii husika. Sasa kama tuliweza kutekeleza hili katika miradi mikubwa, tunaweza pia kulitekeleza kwenye sekta ya uhifadhi,” alisema Deus.

Alitoa mfano wa eneo la Maswa, akisema kuwa kama kuna shughuli za uhifadhi basi watu wanaoishi hapo wanapaswa kunufaika na uwepo wa shughuli hizo.

Mapema, akizungumzia ripoti hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Media Brains Inc, Jesse Kwayu, amesema ripoti hiyo imehusisha nchi nzima, Tanzania Bara na Zanzibar, na kuangazia mambo mengi ambayo ni ukiukwaji wa haki za binadamu na kwamba tayari inapatikana kwa njia ya mtandao.

spot_img

Latest articles

Baraza la saba la Wafanyakazi Wizara ya Nishati lakutana Dodoma

📌 Dkt. Kazungu asema Wizara itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya Kimkakati 📌 Baraza lapitisha rasimu...

Wizara ya Nishati yataja mafanikio utekelezaji majukumu 2024/25

📌 Uzalishaji umeme waongezeka kwa asilimia 59.9 📌 Misheni 300 kuongeza upatikanaji umeme...

Gavana Tutuba: Hali ya uchumi wa Tanzania inaendelea kuimarika

Na Tatu Mohamed GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba amesema kuwa, hali...

Dkt. Biteko: Ufundi Stadi umepewa kipaumbele na serikali

📌 Asisitiza kuwa, Rais Samia anajenga vyuo kila wilaya nchini 📌 Apongeza utoaji wa mafunzo...

More like this

Baraza la saba la Wafanyakazi Wizara ya Nishati lakutana Dodoma

📌 Dkt. Kazungu asema Wizara itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya Kimkakati 📌 Baraza lapitisha rasimu...

Wizara ya Nishati yataja mafanikio utekelezaji majukumu 2024/25

📌 Uzalishaji umeme waongezeka kwa asilimia 59.9 📌 Misheni 300 kuongeza upatikanaji umeme...

Gavana Tutuba: Hali ya uchumi wa Tanzania inaendelea kuimarika

Na Tatu Mohamed GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba amesema kuwa, hali...