Bunge la Kenya laidhinisha kutumiwa kwa Jeshi, Mahakama yaweka ngumu

Nairobi, Kenya

Bunge la Kenya limeidhinisha ombi la Baraza la Ulinzi la kutumiwa kwa Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) kutoa ulinzi kufuatia maandamano ya kupinga Muswada wa Fedha kote nchini. Kulingana na Waraka wa Amri ya Ziada iliyopangwa Jumatano, Juni 26, hatua hiyo itaambatana na Kifungu cha 241 cha Katiba kinachohitaji kuidhinishwa na Bunge kabla ya wanajeshi kutumiwa kushughulikia masuala ya usalama wa ndani.

Hoja hiyo iliwasilishwa Bungeni baada ya ombi kutolewa na Baraza la Ulinzi siku ya Jumatano. “Kwa mujibu wa Kifungu cha 241(3)(c) cha Katiba na vifungu 31(1)(b), 31(1)(c) na 32 vya Sheria ya Majeshi ya Ulinzi ya Kenya, Sura ya 199, Bunge hili linaidhinisha ombi la Baraza la Ulinzi la tarehe 26 Juni 2024 na, kwa maslahi ya usalama wa taifa, IMERIDHIA kutumwa kwa Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) kusaidia Huduma ya Kitaifa ya Polisi katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Kenya yaliyoathiriwa na maandamano ya ghasia yanayoendelea, ambayo yamesababisha uharibifu wa miundombinu muhimu hadi hali ya kawaida irejeshwe,” sehemu ya ilani hiyo ilisema.

Bunge pia limeahirisha vikao vyake vya kawaida hadi Jumanne, Julai 23, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani.

Maandamano hayo, yaliyopewa jina la “Maandamano ya Gen Z,” yamezua ghasia kubwa, ambapo vijana walivamia majengo ya Bunge na kusababisha uharibifu mkubwa na kuchoma sehemu ya bunge hilo.

Mahakama yazuia kutumwa kwa Jeshi

Chama cha Wanasheria nchini Kenya (LSK) kimepata kibali kutoka kwa mahakama kusimamisha serikali kutuma jeshi la KDF kukabiliana na waandamanaji wanaopinga Mswada wa Fedha 2024. Agizo la kutuma jeshi lilichapishwa Jumanne kwenye Gazeti Rasmi la Serikali na kutiwa saini na Waziri wa Ulinzi Aden Duale, na kuzungumziwa na Rais William Ruto kwenye hotuba yake kwa taifa, punde baada ya ghasia kubwa zilizoshuhudiwa na zilizopelekea majengo ya Bunge kuvamiwa.

Hatua hiyo iliibua hisia kali mara moja huku wachanganuzi wakiitaja kuwa kinyume na sheria, wakisema kwamba jeshi linaweza kutumwa tu katika muktadha maalum na kwa idhini ya Bunge. Hata hivyo, Jumatano, Juni 26, 2024 adhuhuri, serikali iliwasilisha hoja bungeni upesi na ikapitishwa chini ya dakika 30, hivyo kuidhinisha kutumwa kwa wanajeshi kudhibiti usalama badala ya polisi wa kawaida.

Kwa kawaida, majukumu ya jeshi ni kulinda taifa dhidi ya wavamizi wanaotishia nchi. Lakini katika hatua inayoonekana kuleta mgogoro mpya, LSK Jumatano alasiri ilipata kibali cha mahakama cha kuzuia serikali kutuma jeshi kwenye barabara za miji kuzima waandamanaji.

“Agizo linatolewa kuzuia washtakiwa wawili (Afisi ya Sheria na Waziri wa Ulinzi), wafanyakazi au maajenti wao kuachilia wanajeshi kutumika katika shughuli za usalama wa nchi kulingana na Tangazo katika Gazeti Rasmi la Serikali nambari 7861 la Juni 25, 2024,” ilisema sehemu ya cheti cha agizo walichopokea LSK.

spot_img

Latest articles

Mchezo wa kuogelea wazidi kupaa nchini, TSA  yafichua siri

Na Winfrida  Mtoi MCHEZO wa kuogelea umezidi kushika kasi nchini  kutokana na kuongezeka idadi ya...

Dkt Nchimbi atembelea banda la Tanesco

Na Mwandishi Wetu MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi...

Waogeleaji chipukizi 400 kutikisa Dar kesho

Na Mwandishi Wetu Zaidi ya waogeleaji 400 wenye umri wa miaka 6 hadi 12 wanatarajiwa...

Wabunge walifuata mkumbo kwenda Morocco kuishangilia Serengeti Boys lawakuta jambo

Na Mwandishi Wetu SPIKA wa Mbunge la Tanzania, Mussa Azzan Zungu ametoa siku nne za...

More like this

Mchezo wa kuogelea wazidi kupaa nchini, TSA  yafichua siri

Na Winfrida  Mtoi MCHEZO wa kuogelea umezidi kushika kasi nchini  kutokana na kuongezeka idadi ya...

Dkt Nchimbi atembelea banda la Tanesco

Na Mwandishi Wetu MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi...

Waogeleaji chipukizi 400 kutikisa Dar kesho

Na Mwandishi Wetu Zaidi ya waogeleaji 400 wenye umri wa miaka 6 hadi 12 wanatarajiwa...