Majaliwa: Taasisi za Umma zitumie mifumo ya Kidigital

*Azindua mifumo minne ya kidijiti Serikalini 

Na Mwandishi Wetu, Media Brains

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezitaka taasisi za umma ziweke mipango madhubuti ya kutumia mifumo ya kidijitali ambayo italeta mageuzi ya kiutendaji na kuifanya Tanzania kuendana na mapinduzi ya nne ya viwanda yanayotumia TEHAMA.

Amesema kuwa mifumo hiyo pamoja na mambo mengine itasaidia kuwabana watumishi wazembe. “Kunahitajika msukumo kuhakikisha mifumo hii inatumika. Niwaelekeze Watendaji Wakuu na watumishi wa umma kuhakikisha mnaandaa mipango na mikakati ya muda mfupi na mrefu ya jinsi mifumo ya kidigitali itakavyotumika kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma kwa umma.”

Amesema hayo leo (Jumapili, Juni 23, 2024) alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika katika viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma. Pia alizindua Mifumo ya Kidijitali ya Uwajibikaji na Usimamizi wa Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma iliyosanifiwa na kujengwa na Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora.

Mifumo iliyozinduliwa ni Mfumo Jumuishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (e-WATUMISHI), Mfumo wa Usimamizi wa Utendaji Kazi (PEPMIS kwa watumishi wa umma na PIPMIS kwa taasisi za umma), Mfumo wa Tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma (HR Assessment) na Mfumo wa e-Mrejesho.

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwaelekeza watendaji wakuu na watumishi wa umma waandae mipango inayopimika. “Mipango hii inapaswa kuwa wazi, yenye malengo yanayopimika na kuzingatia mahitaji ya wananchi na matakwa ya sera za Serikali.”

Katika hatua nyingine, Majaliwa amezitaka taasisi za umma kutoa mafunzo na kuhamasisha matumizi sahihi ya mifumo kwa watumishi wote kwa kuwa ni mipya kwa watumiaji wengi. Ni muhimu kuhamasisha na kuwaelimisha watumishi kuhusu umuhimu wa mifumo hii katika kuboresha huduma kwa umma na kufikia malengo ya Serikali.”

Mapema, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene alisema ubunifu wa mifumo hiyo iliyosanifiwa na kujengwa na Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora umeokoa zaidi ya sh. bilioni 11 ambazo zingetumika kununua mifumo mipya na sh. milioni 616 ambazo zingetumika kila mwka kulipia leseni za mifumo hiyo.

“Mifumo ambayo imekamilika na inasomana, imejengwa na vija25 wa Kitanzania kutoka Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Ofisi ya Rais – Ikulu, Wizara ya Fedha, Wakala wa Serikali Mtandao, Ofisi ya Rais – TAMISEMI na PSRS,” alisema.

Vijana walikabidhiwa vyeti na kutunukiwa tuzo maalumu ili kutambua mchango wao kwa Taifa. 

spot_img

Latest articles

Serikali yazindua shindano la ‘Vijana Uchumi Challenge’ kuibua ubunifu wa vijana

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Nchi ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka,...

Vita ya kusaka tiketi ya China 2026 yanoga, Waogeleaji 200 wachuana vikali

Na Winfrida Mtoi IKIWA ni siku ya pili ya Mashindano ya Taifa ya mchezo wa...

Tanzania yang’ara Tuzo za Utalii Duniani, yaingiza vipengele 41

Na Tatu Mohamed TANZANIA imeendelea kung’ara katika anga la kimataifa baada ya kuingiza vipengele...

Okello awapa jeuri mashabiki wa Yanga

Na Mwandishi Wetu Nyota wa Yanga, Allan Okello amewahakikishia mashabiki wa timu hiyo kuwa watamaliza...

More like this

Serikali yazindua shindano la ‘Vijana Uchumi Challenge’ kuibua ubunifu wa vijana

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Nchi ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka,...

Vita ya kusaka tiketi ya China 2026 yanoga, Waogeleaji 200 wachuana vikali

Na Winfrida Mtoi IKIWA ni siku ya pili ya Mashindano ya Taifa ya mchezo wa...

Tanzania yang’ara Tuzo za Utalii Duniani, yaingiza vipengele 41

Na Tatu Mohamed TANZANIA imeendelea kung’ara katika anga la kimataifa baada ya kuingiza vipengele...