Doyo kugombea uenyekiti ADC, amkaribisha Mchungaji Msigwa

Na Winfrida Mtoi

Katibu Mkuu wa Chama cha  Alliance for Democratic Change (ADC), Doyo Hassan Doyo ametangaza dhamira ya kugombea nafasi ya uenyekiti wa chama hicho Taifa baada ya Hamad Rashid Mohammed kumaliza muda wake.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 6, 2024 jijini Dar es Salaam, Doyo amesema anatangaza kugombea nafasi hiyo kwa kuamini  ana uwezo wa kukitumikia chama hicho katika kutekeleza matakwa ya Katiba.

“Mimi nimejipanga kuwa mwenyekiti wa chama hiki ili kurithi mikoba ya Mheshimiwa  Hamadi Rashid kwa sababu  nimepata mafunzo makubwa sana kutoka kwake. Huyu ni mwanasiasa mzoefu na amefanya kazi na wanasiasa wakongwe,” amesema Doyo.

Amesema Hamad amewafunza jambo katika chama hicho kwani ameonyesha kufuata matakwa ya Katiba kwa  kuachia ngazi baada ya kumaliza muda wake na kuwapa funzo vijana wa chama hicho na wana siasa wengine nchini.

Doyo ameeleza kuwa kati ya mafunzo aliyopata kutoka kwa mwanasiasa huyo mkongwe ni uvumilivu na kupambana na kila changamoto.

Katika hatua nyingine, amemkaribisha Mchungaji Peter  Msigwa wa  Chadema kujiunga na chama hicho endapo haridhishwi na mambo yanavyokwenda huko aliko.

spot_img

Latest articles

Safari ya ‘TLP’ ya Lissu ni ipi?

MWAKA 1992 wakati nchi hii ilipoingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa, kulikuwa...

Karibu 2025, tuyakatae magenge haya sasa

LEO ni siku ya pili katika mwaka mpya wa 2025. Ninawatakia wasomaji wa safu...

Kuubeba uozo wa 2024  kuingia 2025 ni fedheha

NI siku nne tu zimebakia kuupa kisogo mwaka 2024. Mwaka huu ulikuwa na mambo...

Hivi vikosi kazi vimerejea kwa mlango wa nyuma?

KUNA kila dalili kwamba taifa letu kidogokidogo linakumbwa na hali ya kutokuaminiana. Hali hii...

More like this