Na Mwandishi Wetu
WANANCHI Yanga wamejiweka kwenye nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara kwa mara ya tano mfululizo baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Azam FC katika dimba la New Amaan Complex, Zanzibar.
Mabao ya Yanga yamefungwa na Ibrahim Bacca dk 41, Laurindo Depu dk 73, Pacome Zouzoua dk 81. Wanajangwani hao wamefikisha alama 69 katika michezo 28 waliyocheza na kuendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.
Katika mchezo mwingine, Mnyama Simba ameibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa Jamhuri, Morogoro huku akiendelea kusalia nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi akiwa na alama 67 baada ya mechi 28.

Wafungaji wa Simba ni Rushine de Reuck dk 9’p, Selemani Mwalimu dk 77’, Anicent Oura dk 90.
Mechi zilizobaki kwa vigogo hao wa Kariakoo, Yanga itacheza na TRA United nyumbani, kisha JKT Tanzania. Simba itakutana na Singida Bs na KMC, itakuwa nyumbani mechi zote.

Matokeo mengine ya mechi za raundi ya 28
FT: Singida BS 3-1 TZ Prisons (Mossi 2’, 61’, Kennedy 23’ / Sengati 49’)
FT: TRA United 1-1 Coastal Union (Kombo 54’p / Maabad 68’p)
FT: Dodoma Jiji 0-0 JKT Tanzania
FT: Pamba Jiji 0-2 Mbeya City (Ambokile 18’, 76’)
FT: Fountain Gate 0-1 Mashujaa (Hussein Mihambo 86’)
FT: KMC 2-3 Namungo (Mwijage 36’, Mohamed 70’ / Ngoy 18’, 24’, 52’)


