Rais Yanga awatoa hofu mashabiki

Na Winfrida Mtoi

Uongozi wa Klabu ya Yanga umewatoa hofu wadau wa timu hiyo kuwa itaendelea kufanya vizuri kwa kuahidi kuwabakiza wachezaji wote inaowahutaji na kuongeza wengine kuimarisha kikosi.

Hayo yamesemwa na Rais wa klabu hiyo,  Hersi Saidi leo Juni 5, 2024 wakati akizungumza na waandishi wa jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa pamoja na kupata mafanikio makubwa msimu huu, wanajipanga kufanya vizuri zaidi msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Ligi ya Mabingwa Afrika na michuano mingine.

Ameeleza kuwa mafanikio ya msimu huu yametokana na kujitoa kwa dhati kwa wachezaji wao na uongozi mzima wa benchi la ufundi.

“Niwapongeze wachezaji wetu, kazi kubwa mmeifanya, Kuanzia leo tunawapa wachezaji wetu likizo ya mwezi mmoja, tutakutana nao tena mwanzoni mwa mwezi wa saba wa  kujiandaa na msimu mpya ambapo tutakuwa tayari tumefanya usajili wa kuimarisha kikosi chetu,” amesema Hersi.

Msimu huu Yanga imefanikiwa  kutetea mataji yake mawili la Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho la TFF, huku michuano ya Kimataifa ikifika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

spot_img

Latest articles

MAB yateta na wadhibiti Mutukula OSBP

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa TMDA (MAB), Eric Shitindi...

Rais Samia: Hakuna mtoto atafika darasa la tatu bila kujua kusoma, kuandika na kuhesabu

Na Tatu Mohamed RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan,...

Uwanja wa KMC wafungiwa

Na Mwandishi Wetu  SHIRIKISHO la Soka Tanzania, (TFF) limeufungia uwanja wa KMC, uliopo Mwenge, jijini...

More like this

MAB yateta na wadhibiti Mutukula OSBP

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa TMDA (MAB), Eric Shitindi...

Rais Samia: Hakuna mtoto atafika darasa la tatu bila kujua kusoma, kuandika na kuhesabu

Na Tatu Mohamed RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan,...