Na Mwandishi Wetu
Nyota mpya wa Yanga, Albert Kangwanda amewapa raha mashabiki wa timu hiyo baada ya kufunga bao lilowapa Waanchi hao taji la Ngao ya Jamii mbele ya watani wao wa jadi Simba kwa ushindi wa 1-0 kwenye dimba la New Amaan Complex, Zanzibar.
Yanga inatwaa Ngao ya Jamii kwa mara ya tatu mfululizo, msimu uliopita iliifunga Simba 1-0, mwaka 2024 iliifunga Azam FC 4-1.
Wanajangwani hao kwa sasa wanafikisha mataji 10, sawa na Simba tangu michuano hiyo ilipoanzishwa mwaka 2001.


