Kanda ya Ziwa , Kaskazini vinara mauaji ya mapenzi

Kanda ya Kaskazini na Kanda ya Ziwa nchini imetajwa kuwa ni vinara wa matukio ya mauaji ya wapenzi kutokana na wivu wa mapenzi.

Taarifa ya haki za binadamu ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) ya mwaka 2023 iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam jana, ilisema kuwa vifo 50 vya wapenzi kuuana vilivyoripotiwa nchini kote mwaka jana.

Katika idadi hiyo, asilimia 50 ya vifo hivyo viliripotiwa kutoka Kanda hizo. Kanda ya Kaskazini inayojumuisha mikoa ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga, wakati Kanda ya Ziwa inajumuisha Kagera, Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Geita na Mara. Idadi ya vifo vingine vimeripotiwa kutoka kanda nyingine tano zilizoko nchini.

Ripoti ya haki za binadamu ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) ya mwaka 2023 iliyozinduliwa jana, imeeleza kuwa mauaji hayo yameongezeka kutoka vifo 33 yaliyoripotiwa mwaka 2022.

Katika mchanganuo wa mauaji hayo, wanawake waliouawa ni 45 sawa na asilimia 90 ya vifo hivyo, wakati wanaume waliouawa ni watano sawa na asilimia 10 ya matukio hayo yanayozidi kuongezeka nchini kila mwaka, mwaka jana ukiwa umeshuhudia ongezeka vifo 17.

Taarifa hiyo inaonyesha kuwa tangu mwaka 2019 hadi mwaka jana, watu waliouawa kutokana na migogoro ya kimapenzi ni 162, licha ya idadi hiyo kuwa kubwa, inahofiwa kwamba yapo matukio mengine mengi ya mauaji ya aina hiyo ambayo yalitokea, lakini hayakutolewa taarifa.

Kwa mujibu wa LHRC asilimia 46 ya vifo vyote vilisababishwa na wivu wa mapenzi. Sababu nyingine za mauaji hayo, ni wapenzi kutokutaka kuendelea kuwa pamoja, hasa wanawake, migogoro ya ndoa na ugomvi wa mali.

Katika ripoti hiyo inayopitia matukio mbalimbali kuhusu haki za binadamu nchini kwa mwaka 2023, pia inataja mauaji ya vyombo vya dola kuua raia kuwa yalipungua kutoka vifo 10 mwaka 2022 hadi vifo 7; huku vifo vilivyosababishwa na mauaji ya imani za kishirikina vikiwa ni 164 kwa mwaka 2023; wananchi kujichukulia sheria mkononi ilisababisha vifo 461 vikipungua kutoka vifo 473 vya mwaka 2021.

Ripoti hiyo pia imezungumzia athari kwa haki za binadamu katika masuala ya ukatili wa wanawake na watoto; haki jina; ukatili dhidi ya wazee; ukatili kutokana na imani za kishirikina manusura wengi wakiwa ni wanawake; mabadiliko ya tabia nchi; utesaji; rushwa na utawala mbaya, matumizi mabaya madaraka na rasilimali za umma; haki ya mali na masuala ya bima ya afya.

spot_img

Latest articles

Neema Mchau ajitosa kugombea Udiwani Viti Maalum Ilala

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Gongolamboto Neema Mchau amechukua fomu...

Amanzi na Babu Tale uso kwa uso Jimboni

Na Mwandishi Wetu ALIYEKUWA Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Tawi la Chuo...

VETA Pwani yabuni Mita ya Maji ya Kisasa, kutatua migogoro kwa wapangaji

Na Tatu Mohamed KATIKA hatua ya kuleta mageuzi katika usimamizi wa matumizi ya maji...

Ofisi ya Msajili Hazina yazitaka taasisi za umma kutumia maonesho ya Sabasaba kutangaza huduma

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili Hazina yazitaka taasisi za umma kutumia maonesho ...

More like this

Neema Mchau ajitosa kugombea Udiwani Viti Maalum Ilala

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Gongolamboto Neema Mchau amechukua fomu...

Amanzi na Babu Tale uso kwa uso Jimboni

Na Mwandishi Wetu ALIYEKUWA Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Tawi la Chuo...

VETA Pwani yabuni Mita ya Maji ya Kisasa, kutatua migogoro kwa wapangaji

Na Tatu Mohamed KATIKA hatua ya kuleta mageuzi katika usimamizi wa matumizi ya maji...