Wanafunzi saba wa Shule ya Msingi Ghati Memorial wanahofiwa kufariki dunia baada ya gari la shule waliokuwemo kuangukia kwenye korongo lililojaa maji eneo la Dampo, Kata ya Muriet mkoani Arusha.
Korongo hilo limejaa maji yaliyotokana na mvua kubwa iliyonyesha usiku usiku wa kuamkia leo April 12, 2024, ilisababisha maji kujaa hadi barabarani.
Wakizungumza katika eneo la tukio, mashuhuda wamesema kuwa saa 12 asubuhi, gari lenye namba za usajili T 496 EFK lilikatiza juu ya barabara hiyo, dereva alishindwa kulidhibiti, hivyo liliyumba kabla ya kuangukia katika korongo hilo linalomwaga maji yake katika mto mkubwa wa Themi.
Mmoja wa mashuhuda amesema baada ya watu kuona hali hiyo walisogea eneo la tukio na kufanikiwa kuokoa watoto wanne kabla ya gari kuendelea kusogea tena na watoto wengine walionekana kusombwa na maji.“Dereva alipoona gari linamshinda aliruka ndio watu wakaona wakaanza kusaidia hao watoto, lakini gari lilizidi kusogea kwenye kina tukaamua kuita Jeshi la Zimamo.
Chanzo: Mwananchi