Rais mstaafu Brazil matatani kwa udanganyifu vipimo vya COVID 19

Polisi wa nchini Brazil wanapendekeza kwamba Rais wa zamani wa nchi hiyo, Jair Bolsonaro ashtakiwe kwa makosa ya jinai, baada ya uchunguzi wao kubaini kufanyika kwa mabadiliko ya rekodi za chanjo ya Covid-19 ili kumnufaisha kiongozi huyo na wanafamilia wa karibu.

Jaji wa Mahakama ya Juu ya nchini humo, Alexandre de Moraes jana Jumanne aliweka hadharani ripoti ya uchunguzi wa polisi, ambayo inamtuhumu rais huyo wa zamani kujihusisha na uhalifu pamoja na kutoa data zenye udanganyifu, baada ya vyombo vya habari vya ndani kuripoti juu ya mashtaka yake.

Uamuzi huo unakuja mwaka mmoja baada ya polisi kuvamia nyumba ya Bolsonaro ili kuchunguza ikiwa data za uwongo ziliingizwa kwenye hifadhidata ya wizara ya afya ili kupata uthibitisho wa chanjo ya Bolsonaro na familia yake kabla ya safari za kimataifa. Bolsonaro hajazungumza chochote hadharani kuhusu tuhuma hilo, lakini aliwahi kukanusha kuhusika na makosa yoyote katika utawala wake.

Hata hivyo Fabio Wajngarten ambaye ni msemaji na wakili wake, alisema katika chapisho la mtandao wa kijamii kwamba shtaka hilo ni “upuuzi” na akalalamika kuwa upande wa utetezi haujaiona taarifa hiyo ya uchunguzi wa polisi.

Polisi wanasema Bolsonaro alimwamuru Luteni Kanali Mauro Cid Barbosa kupata rekodi za kugushi za chanjo kwa ajili yake na binti yake mara tu alipojua kwamba afisa huyo, ambaye alikuwa Katibu wake binafsi wakati huo, alikuwa amejitengenezea hati kama hiyo. Mamlaka zinadai kuwa mfumo huo wa afya uliingiliwa na kuchapisha vyeti vya chanjo vya kugushi kutoka Ikulu ya Rais.

Ripoti ya polisi kwa sehemu imeegemea kwenye ushahidi uliotolewa na Cid Barbosa ambaye alikamatwa Mei mwaka jana, lakini akaachiwa baada ya kusaini makubaliano (plea bargain) na wachunguzi wa kesi hiyo.

Watu 17 akiwamo Bolsonaro na Cid Barbosa wamefunguliwa mashtaka na polisi wa shirikisho jana. Hatua hiyo inaipeleka kesi katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Brazili, ambaye ataamua iwapo aendelee moja kwa moja na mashtaka husika, kuomba uchunguzi wa ziada au kufunga kesi hiyo. Ikiwa kesi hiyo itaamriwa kuendelea, itasikilizwa na Mahakama ya Juu, ambayo hatimaye inaweza kumtia hatiani

spot_img

Latest articles

Soma Ripoti ya UHIFADHI WA UHAI: UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU NDANI YA SEKTA YA UHIFADHI TANZANIA

Na Mwandishi Wetu, Media Brains Utafiti mpya umebaini kwamba mamlaka za serikali zimekuwa kichocheo kikuu...

RAIS DKT. SAMIA ATOA MAAGIZO KWA BASHE, NFRA KUNUNUA MAHINDI KWA WAKULIMA TSH 700 KWA KILO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassanamemuagiza Waziri wa Kilimo...

Upi upepo unaoweza kufika Tanzania,wa Wiliam Ruto au Paul Kagame?

KUNA upepo wa aina mbili unavuma katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mmoja...

Watu wawili wafariki, 16 wajeruhiwa katika ajali ya basi Songwe

Na Mwandishi Wetu, Media Brains Watu wawili wamefariki dunia na wengine 16 kujeruhiwa baada ya...

More like this