Sehemu kadhaa nchini zimekumbwa na ‘giza’ kwa saa kadhaa leo Jumatatu Machi 4, 2024, baada ya umeme kukatika kutokana na kile ambacho Shirika la Umeme Tanzania [TANESCO] limekitaja kuwa ni hitilafu iliyotokea katika gridi ya Taifa.
Taarifa iliyotolewa na Tanesco imesema hitilafu hiyo ingesababisha kukosekana kwa umeme kwa baadhi ya maeneo ya Tanzania Bara na Zanzibar.”Shirika linawaomba radhi kwa usumbufu wowote utakao jitokeza”, inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.
Kwa upande mwingine, Mtandao wa Millardayo umelinukuu Shirika la Umeme Zanzibar [ZECO] likisema Zanzibar nzima imekosa umeme kuanzia saa 7 mchana wa leo kutokana na hitilafu iliyotokea Tegeta, Dar es Salaam.
“Mpendwa mteja kuna hitilafu ya umeme mkubwa mkondo wa kilovolti 132 kutoka Tegeta Bara kuja Zanzibar kuliko sababisha kuzimika umeme hafla maeneneo yote ya Zanzibar. Zeco inaomba radhi kwa usumbufu unaoendelea kujitokeza ahsante,” ZECO