PSSSF yapewa siku 100 kukamilisha ujenzi kiwanda cha ngozi

Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhandisi Cyprian Luhemeja ametoa siku 100 kwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Wafanyakazi wa Umma (PSSSF) kuhakikisha awamu ya pili ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata bidhaa za ngozi Kilimanjaro unakamilika na kuanza kufanya kazi ifikapo Julai 2024.

Agizo hilo amelitoa leo Februari 22,2024 alipofanya ziara ya kukagua ujenzi katika kiwanda cha bidhaa za ngozi Kilimanjaro International Leather Industries Ltd (KLICL) ikiwa ni sehemu ya kukagua maendeleo ya miradi inayotekelezwa na serikali kupitia ofisi hiyo.

Mhandisi Luhemeja amesema kukamilika kwa kiwanda hicho kutaongeza thamani ya zao la ngozi ghafi, kufungua fursa za soko la uhakika la ngozi kutoka kwa wafugaji, kuongeza ajira kwa vijana na mapato ya fedha za ndani na za kigeni.

Aidha, amefurahishwa na ubora wa bidhaa zinazozalishwa kiwandani hapo na kutoa wito kwa Watanzania kuwa na tamaduni za kuthamini bidhaa zinazozalishwa nchini.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Abdul-Razaq Badru, amesema amepokea maagizo hayo na kuahidi kuwa watashirikiana na Jeshi la Magereza kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi kama ilivyoelekezwa ili Watanzania waanze kunufaika na mradi huo.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho, Mhandisi Saiba Edward, amesema mradi huo utaongeza kipato kwa wakazi wa Kilimanjaro na mikoa jirani kupitia fursa za uzabuni, uwakala na usambazaji wa bidhaa.

Kwa upande wake Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Frank Mwakijungu, amesema Magereza ni mbia wa utekelezaji mradi huo hivyo watasimamia ujenzi wa kiwanda hicho ili kikamilike kwa wakati kwa manufaa ya Watanzania.

spot_img

Latest articles

Dk. Mwigulu: Tutamuenzi kwa vitendo marehemu Jenista

Na Mwandishi Wetu WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba amesema Serikali itayaendeleza mambo yote mema yaliyofanywa na...

Balozi Bandora kuzikwa kesho makaburi ya Kinondoni

Mwanadiplomasia nguli wa Tanzania, aliyewahi  kuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria na Mratibu Mkazi...

Serikali yajipanga kuimarisha utumishi wa umma, kuendeleza mageuzi ya kidigitali

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa...

Bokya amtahadharisha mapema Tyson wa Bongo

Na Winfrida Mtoi Bondia Ismail Khalid maarufu Boyka ametamba kutoa kipigo kikali kwa mpinza wake...

More like this