Watalii zaidi ya 2,000 watua nchini na meli ya Kitalii

Na Shani Nicolaus, Media Brains

Meli kubwa iliyobeba watalii 2,210 kutoka Canada, imewasili alfajiri ya leo Jumanne Januari 16, 2024 katika Bandari ya Dar es Salaam.

Meli hiyo maarufu kama Norwegian Cruise Line Dawn yenye urefu wa mita 294, imetajwa kuwa kubwa zaidi kuwasili katika bandari zote nchini Tanzania tangu kuanzishwa kwake.

Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Mrisho Mrisho amewaambia wanahabari mapema leo kuwa hadi inafika Tanzania, meli hiyo imepitia katika bandari tofauti ikiwemo ile ya Mombasa, nchini Kenya na ina uwezo wa kubeba abiria 4,700, japo waliowasili ni watalii 2,210 pamoja na wafanyakazi zaidi ya 1,000.

Norwegian Cruise Line Dawn ilianza kufanya kazi mwaka 2002 ikiwa na thamani ya zaidi ya Sh trilioni 1, ina kimo cha mita 59, ikienda kwa kasi ya kilomita 46 kwa saa na ina wafanyakazi zaidi ya 1,000.

Rekodi zinaonyesha kuwa mara ya mwisho kwa meli ya kitalii kutia nanga katika Bandari ya Dar es Salaam, ilikuwa Novemba 10, 2022, ambapo meli ya Zaandam inayomilikiwa na Kampuni ya Holland American Line ilitia nanga kwa siku mbili kabla ya kuelekea visiwani Zanzibar, ikiwa na watalii 1,500.

Aidha, Aprili 8, 2022 Bandari ya Dar es Salaam ilipokea meli kubwa aina ya Frontier Ace iliyobeba magari 4,041 ikiwa ni ya kwanza kubeba mzigo mkubwa wa magari tangu kuanzishwa kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).

Upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Damas Mfugale amesema watalii waliokuja na meli hiyo watatembelea mji wa kihistoria ya Bagamoyo, wengine watakwenda Hifadhi ya Selous kwa ajili ya kutazama wanyama na wengine watafanya utalii katika jiji la Dar es Salaam.

“Hii ni hatua ya muhimu kwenye uchumi wa utalii, tunatarajia kila watakapo pita Watanzania watanufaika,” amesema Mfugale.

Sehemu ya watalii hao waliokuja na meli hiyo, Suzanne Ramage na Gem Cheesman kutokana Canada, wamesema wanafuraha kufika Tanzania ikiwa ni mara yao ya kwanza.

spot_img

Latest articles

Chondechonde Polisi msisababishe wananchi wakate tamaa

ALHAMISI iliyopita yaani Desemba 5, mwaka huu wa 2024 lilitokea tukio baya la kuhuzunisha...

Ufaransa yaipatia Tanzania Sh bilioni 323.4

Na Mwandishi Wetu Serikali ya Tanzania na Shirika la Maendeleo La Ufaransa (AFD) wamesaini mikataba...

TANZANIA YAWEKA REKODI MKUTANO WA WAHASIBU WAKUU AFRIKA

Na Mwandishi Wetu Tanzania imeweka rekodi ya Mkutano wa Pili wa Wahasibu Wakuu wa Serikali...

TANZANIA KUPAMBANA NA JANGWA

Na Mwandishi wetu Serikali imejipambanua katika kupambana na kuenea kwa jangwa, kurejesha ardhi iliyoharibiwa pamoja...

More like this

Chondechonde Polisi msisababishe wananchi wakate tamaa

ALHAMISI iliyopita yaani Desemba 5, mwaka huu wa 2024 lilitokea tukio baya la kuhuzunisha...

Ufaransa yaipatia Tanzania Sh bilioni 323.4

Na Mwandishi Wetu Serikali ya Tanzania na Shirika la Maendeleo La Ufaransa (AFD) wamesaini mikataba...

TANZANIA YAWEKA REKODI MKUTANO WA WAHASIBU WAKUU AFRIKA

Na Mwandishi Wetu Tanzania imeweka rekodi ya Mkutano wa Pili wa Wahasibu Wakuu wa Serikali...