Warning: Array to string conversion in /home/themedia/domains/themediabrains.com/public_html/wp-includes/shortcodes.php on line 434
Array

Majaliwa: Viongozi wa Dini wahamasisheni Vijana kufanya kazi kwa weledi

Na Mwandishi Wetu, Media Brains

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ametoa wito kwa viongozi wa dini kuwahimiza vijana kufanya kazi kwa staha, weledi na uadilifu ili kuzitumia rasilimali zilizopo nchini kujiletea maendeleo.

“Nchi yetu imebarikiwa fursa nyingi za kiuchumi, ili jamii ione matunda ya uwepo wa fursa hizo tunategemea sana nguvu kazi ya vijana katika kuzitumia rasilimali zilizopo,” amesema.

Ametoa wito huo Jumapili Oktoba 01, 2023 wakati wa Jubilei ya miaka 125 ya Uinjilishaji katika Jimbo Kuu Katoliki la Songea, kwenye kilima cha Peramiho, Songea mkoani Ruvuma.

Aidha, amezisihi Taasisi za dini kuweka mipango mahsusi na shirikishi ya malezi ya vijana. “Tumieni nafasi zenu kuongeza msukumo wa malezi kwa vijana kwa kuweka mifumo ya kuwafuatilia kwa karibu na kuhimiza ushiriki wao kwenye vyama vya kitume,” amesema Mjaliwa.

Kadhalika, Majaliwa amewasihi viongozi wa dini waendelee kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa masuala ya kipaumbele yanayohusu ustawi wa Taifa. 

“Niwasihi sana mtuunge mkono kuhamasisha uhifadhi wa mzingira na matumizi ya nishati safi, kampeni za kupanda miti na usafi wa mazingira, kukemea vikali vitendo vya mmomonyoko wa maadili, matumizi ya madawa ya kulevya na kukemea vitendo vya rushwa,” amesema Majaliwa.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameyapongeza madhehebu ya dini kwa kuendelea kutoa huduma mbalimbali za kijamii kwenye sekta za elimu, afya, maji na huduma nyingine za kijamii hasa katika maeneo ya pembezoni.

“Kazi hiyo mnayoifanya ya kutoa huduma kwa jamii ni kuunga mkono dhamira ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuboresha ustawi wa jamii ya Watanzania kwa kusogeza huduma zote muhimu karibu na wananchi,” amesema Majaliwa.

Katika Jubilei hiyo, Rais Dk. Samia ametoa shilingi milioni kumi kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 125 ya jubilei ya Uinjilishaji katika jimbo kuu Katoliki la Songea.

Naye, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Songea Damian Dallu ameishukuru Serikali kwa ushirikiano inaoutoa katika shughuli mbalimbali za huduma za jamii na uinjilishaji zinazofanywa na kanisa katoliki nchini.

spot_img

Latest articles

Yacouba atambulishwa Mbeya City

Na Mwandishi Wetu NYOTA wa zamani wa Yanga, raia wa Burkina Faso, Yacouba Songne, ametambulishwa ...

Waziri Ndejembi: Tanzania ina fursa kubwa ya kuendeleza nishati ya Jotoardhi

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi, amesema kutokana na uwepo wa vyanzo...

‘Guardians of the Peak’ kuinua utangazaji utalii wa Kilimanjaro kupitia filamu

Na Mwandishi Wetu MRADI wa Guardians of the Peak, unaoingia msimu wake wa pili,...

Serikali yazindua Jukwaa la Vijana, yataja vijana kuwa mhimili Mkuu wa Maendeleo ya Taifa

Na Tatu Mohamed SERIKALI imezindua rasmi jukwaa la kitaifa la vijana lijulikanalo kama ‘Vijana...

More like this

Yacouba atambulishwa Mbeya City

Na Mwandishi Wetu NYOTA wa zamani wa Yanga, raia wa Burkina Faso, Yacouba Songne, ametambulishwa ...

Waziri Ndejembi: Tanzania ina fursa kubwa ya kuendeleza nishati ya Jotoardhi

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi, amesema kutokana na uwepo wa vyanzo...

‘Guardians of the Peak’ kuinua utangazaji utalii wa Kilimanjaro kupitia filamu

Na Mwandishi Wetu MRADI wa Guardians of the Peak, unaoingia msimu wake wa pili,...