Jeshi la polisi kuendelea kutumia TEHAMA katika kupambana na uhalifu nchini

Na Mwandishi Wetu, Media Brains

Jeshi la Polisi limesema litaendelea kutumia Tehama na mifumo katika kupambana na uhalifu wa kimtandao hapa Nchini,kutokana na Mabadiliko ya sayansi na Teknolojia na Ulimwengu wa sasa ambao wahalifu wamekuwa wakiutumia kutenda uhalifu.

Hayo ameyasema leo Agosti 17,2023 na Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA) Kamishna msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP Dk. Lazaro Mambosasa wakati akipokea Kompyuta kutoka kwa kampuni ya Sura Technologies Company Limited ya jijini Dar es Salaam ambapo amebainisha kuwa kompyuta hizo zitasaidia katika ufundishaji kwa askari walioko katika mafunzo.

Dk. Mambosasa amebainisha kuwa kompyuta hizo ni za kisasa ambazo zitawasaidia wakufunzi katika kufundisha wanafunzi waliopo katika chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA) huku akitoa rai kwa wanafunzi kutumia vifaa hivyo vizuri ili viwanufanishe katika kupata mafunzo ya Tehama ambayo ndio dira ya Dunia kwa sasa.

Kwa upande wake, Edmund Mbao kutoka Sura Technologies Company Limited amesema kuwa wao kama wadau wa kupinga maswala ya kihalifu waliona ni vyema watoe vifaa hivyo vya Tehama kwa Jeshi la Polisi ambalo linahusika moja kwa moja na mapambano ya uhalifu hapa Nchini ambapo amebainisha kuwa wanaamini vifaa hivyo vinakwenda kutumika katika kufundisha askari ambao watapata mafunzo ya Tehama ili kukabiliana na uhalifu wa kimtandao hapa Nchini.

Naye Mkufunzi Mkuu wa chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam, Kamishna msadizi wa Polisi ACP Andrea Legembo amesema kuwa kompyuta hizo zitakwenda kuongeza ufanisi wa ufundishaji wa Tehama kwa wanafunzi na wakufunzi wa chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA).

spot_img

Latest articles

Ndumbaro: Sheria 300 Zimetafsiriwa kwa Kiswahili Ili Kuimarisha Uelewa kwa Wananchi

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro, amesema kuwa hadi...

Jessica: CCM inajali uongozi wa vijana

Na Mwandishi Wetu KATIBU wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM TAIFA, Jessica Mshama...

Waziri Aweso: Tuna uhakika wa maji ya kutosha Dar na Pwani

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amewatoa hofu wakazi wa mikoa ya...

PURA yajivunia mafanikio katika Ajenda ya Nishati Safi na ushiriki wa Watanzania Sekta ya Mafuta na Gesi

Na Tatu Mohamed MAMLAKA ya Kudhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imesema inajivunia...

More like this

Ndumbaro: Sheria 300 Zimetafsiriwa kwa Kiswahili Ili Kuimarisha Uelewa kwa Wananchi

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro, amesema kuwa hadi...

Jessica: CCM inajali uongozi wa vijana

Na Mwandishi Wetu KATIBU wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM TAIFA, Jessica Mshama...

Waziri Aweso: Tuna uhakika wa maji ya kutosha Dar na Pwani

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amewatoa hofu wakazi wa mikoa ya...