Warning: Array to string conversion in /home/themedia/domains/themediabrains.com/public_html/wp-includes/shortcodes.php on line 434
Array

Madaktari wafanikiwa kukiongezea damu kijusi ndani ya tumbo la mama

Nairobi, Kenya

Madaktari katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta nchini Kenya wamefanikiwa kutia damu kwa kijusi akiwa bado kwenye mfuko wa uzazi wa mama huyo.

Utaratibu huo wa umakini zaidi, unaojulikana kama Uhamisho wa Ndani wa Kijusi ni hatua muhimu katika matibabu ya kijusi na utaalamu wa tiba ya ndani ya mwili wa mama.

Timu ya madaktari bingwa wanne walifanya utaratibu huo wa kimatibabu ambapo chembe nyekundu za damu kutoka kwa wafadhili hudungwa ndani ya kijusi.

Uhamisho wa ndani ya mfuko wa uzazi unaweza kupendekezwa wakati kijusi kina upungufu wa damu au Anemia (hali inayopunguza seli za damu).

Madaktari hao ni pamoja na Rosa Chemwey, Flavia Ogutu, Ikol Adung’o na Kunjira Murayi, Mtaalamu wa tiba ya miale.

Walisaidiwa na Benson Nyankuru na Redempata Mumo ambao ni wauguzi, na Tony Wainaina, Afisa wa Kliniki ya Afya ya Uzazi.

Kwa kutumia kipimo cha ultrasound ili kubainisha nafasi ya kijusi na na kondo la nyuma la uzazi, daktari wa upasuaji huingiza sindano kwenye fumbatio la mama na kisha kwenye mshipa wa kitovu cha kijusi.

spot_img

Latest articles

Baba Levo atembelea Banda la TTCL Sabasaba, apongeza Mapinduzi ya Kidijitali

Na Mwandishi Wetu MSANII na mtangazaji maarufu nchini, Clayton Chipando maarufu kama Baba Levo,...

Takwimu za Samia ni nzito, kupotezwa watu akaze zaidi

IJUMAA ya wiki iliyopita yaani Juni 27, 2025 Rais Samia Suluhu Hassan aliweka historia...

Maonesho ya Sabasaba kufunguliwa Julai 7 na Rais Mwinyi

Na Tatu Mohamed RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinzudi, Dkt. Hussein...

TTCL Yajipambanua Kama Muunganishaji Thabiti wa Mawasiliano Sabasaba 2025

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeendelea kudhihirisha uwezo wake...

More like this