Wananchi Kibakwe wamuomba Simbachawene kusaidia kuwapata walengwa wa TASAF

Na Mwandishi Wetu, Media Brains

Wananchi wa Kata ya Malolo iliyopo Jimbo la Kibakwe katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma wamepaza sauti zao kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene wakimuomba asaidie kubadili mchakato wa kuwapata walengwa halisi wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) huku wakisisitiza kuwa utaratibu unaotumika kwa sasa umegubikwa na sintofahamu.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene akipokea taarifa ya Kijiji cha Idodoma kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Hashimu Kolezani wakati wa mkutano wake wa hadhara na wananchi wa Kijiji hicho uliolenga kuelezea changamoto mbalimbali  za kijiji  ikiwemo namna ya kuwabaini walengwa wa TASAF, Ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kikazi za kijiji kwa kijiji kwa ajili ya kuzungumza na wanachi wa Jimbo hilo la Kibakwe analoliongoza.

Aidha, Wananchi hao wamewataka walengwa wa Mpango huo ambao tayari wameimarika kiuchumi kuwa na utu kwa kujiondoa na kuwapisha wengine wanaostahili kuingizwa kwenye Mpango.

Hayo yameelezwa Julai 18, 2023 na wananchi mbalimbali kwa nyakati tofauti kupitia mikutano ya hadhara ya Waziri huyo anayoendelea kuifanya katika Vijiji vya Jimbo la Kibakwe ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ambapo wananchi hao wameomba ubainishaji huo wa walengwa ufanyike kwa uwazi ikiwezekano kupitia mikutano ya hadhara ili waweze kuwapata walengwa halisi.

Wamefafanua kuwa licha ya TASAF kuwashirikisha viongozi wa vijiji husika katika kuwabaini Walenga halisi lakini bado hawaridhishwi na jinsi mchakato unavyoendeshwa kwani kuwekuwa na usiri wa hali ya juu.

Wamesema kuwa mchakato huo katika ngazi za vijiji haufanyiki vizuri hivyo kupelekea wale ambao sio maskini halisi kuwa wanufaika ilhali wale maskini halisi wakiendelea kutaabika.

Malalamiko hayo ya wananchi yalitokana na maswali ya Mhe. Simbachawene ya kutaka kuwatambua walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Kata hiyo ya Malolo na namna walivyopatikana ili kujiridhisha na minongóno aliyoisikia juu ya upatikanaji wa walengwa hao.

Akijibu malalamiko hayo, Waziri Simbachawene amesema tayari ameshatoa maelekezo kwa Menejimenti ya TASAF Makao Makuu kuangalia namna bora ya kuwapata walengwa halisi wa Mpango.

Ameongeza kuwa TASAF msingi wake ni mpango shirikishi wa kuondoa umasikini uliokithiri kwa wananchi, hivyo ni lazima kutafuta njia sahihi ili  kutimiza azma ya kuanzishwa kwake.

spot_img

Latest articles

Soma Ripoti ya UHIFADHI WA UHAI: UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU NDANI YA SEKTA YA UHIFADHI TANZANIA

Na Mwandishi Wetu, Media Brains Utafiti mpya umebaini kwamba mamlaka za serikali zimekuwa kichocheo kikuu...

RAIS DKT. SAMIA ATOA MAAGIZO KWA BASHE, NFRA KUNUNUA MAHINDI KWA WAKULIMA TSH 700 KWA KILO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassanamemuagiza Waziri wa Kilimo...

Upi upepo unaoweza kufika Tanzania,wa Wiliam Ruto au Paul Kagame?

KUNA upepo wa aina mbili unavuma katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mmoja...

Watu wawili wafariki, 16 wajeruhiwa katika ajali ya basi Songwe

Na Mwandishi Wetu, Media Brains Watu wawili wamefariki dunia na wengine 16 kujeruhiwa baada ya...

More like this

Soma Ripoti ya UHIFADHI WA UHAI: UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU NDANI YA SEKTA YA UHIFADHI TANZANIA

Na Mwandishi Wetu, Media Brains Utafiti mpya umebaini kwamba mamlaka za serikali zimekuwa kichocheo kikuu...

RAIS DKT. SAMIA ATOA MAAGIZO KWA BASHE, NFRA KUNUNUA MAHINDI KWA WAKULIMA TSH 700 KWA KILO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassanamemuagiza Waziri wa Kilimo...

Upi upepo unaoweza kufika Tanzania,wa Wiliam Ruto au Paul Kagame?

KUNA upepo wa aina mbili unavuma katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mmoja...