Waziri Ndejembi awasilisha bajeti ya 2026/26, kipaumbele umeme wa uhakika nchini

Na Mwandishi Wetu


Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi, amewasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2026/2027, akiainisha vipaumbele katika sekta ndogo ya umeme kuwa ni pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa ajili ya kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Akisoma hotuba ya bajeti hiyo Aprili 22, 2026, Bungeni Dodoma, Waziri Ndejembi ametaja vipaumbele hivyo kuwa ni pamoja na kuendeleza uzalishaji wa umeme kupitia mitambo tisa katika Kituo cha Kufua Umeme cha Bwawa la Julius Nyerere.

Pia kukamilisha awamu zinazofuata katika mradi wa kuzalisha umeme kwa nguvu ya jua Kishapu baada ya megawati 50 kuunganishwa kwenye gridi ya taifa na utekelezaji wa mradi wa umeme wa Malagarasi, Kigoma unaotarajia kuzalisha Megawati 49.5 za umeme.

Akizungumzia mafanikio yaliyopatikana katika eneo la uzalishaji umeme, Waziri Ndejembi amesema hadi kufikia mwezi Machi 2026, uwezo wa kuzalisha umeme umeongezeka na kufikia jumla ya megawati 4,522.54 kutoka megawati 4,031.71 mwaka2025 ikiwa ni ongezeko la asilimia 12.17

Amesema ongezeko hili limetokana na kukamilika kwa miradi mbalimbali ya umeme, ukiwemo mradi wa kuzalisha umeme kwa nguvu ya jua Kishapu (awamu ya kwanza) unaozalisha jumla ya megawati 50.

Aidha, katika eneo la usafirishaji, amesema hadi kufikia mwezi Machi 2026, urefu wa miundombinu ya kusafirisha umeme nchini ulikuwa umefikia jumla ya kilomita 8,500.38 kutoka kilomita 7,809.67 mwezi Machi 2025.

“Hadi kufikia Machi 2026, urefu wa miundombinu ya kusafirisha umeme nchini ulikuwa umefikia kilomita 8,500.38 ikilinganishwa na kilomita 7,809.67 zilizokuwepo Machi 2025, sawa na ongezeko la asilimia 9,” alisema.

Amesisitiza kuwa Serikali, kupitia TANESCO, imeendelea kuimarisha huduma kwa wateja kwa kuboresha mifumo ya kidijitali, ambapo ilizindua mita janja (smart meters) zinazowezesha umeme ulionunuliwa na mteja kuingia moja kwa moja kwenye mita.

“Hadi kufikia Machi 2026, jumla ya wateja 105,739 walikuwa wameunganishwa na mita janja, na zoezi hilo linaendelea kwa awamu katika maeneo yote ya nchi,” alieleza Mhe. Ndejembi.

Waziri Ndejembi pia amefafanua kuwa kutokana na hatua zilizochukuliwa katika ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji na usambazaji wa umeme, kiwango cha upatikanaji wa umeme nchini kimeongezeka kutoka wastani wa asilimia 78.4 mwaka 2020 hadi kufikia wastani wa asilimia 85.5.

spot_img

Latest articles

Sangweni: Sekta ya Mafuta na Gesi Ni Chachu ya Ukuaji wa Uchumi wa Taifa

Na Mwandishi Wetu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli...

VETA Kihonda yaja ‘cold room’ kupunguza upotevu wa mazao ya wakulima

Na Mwandishi Wetu UBUNIFU wa mfumo jumuishi wa kuhifadhi mazao kwa kutumia teknolojia ya ubaridi...

Ofisi ya Msajili wa Hazina yalenga kukusanya Sh2 trilioni mwaka 2026/27

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) imejiwekea lengo la kukusanya Sh2...

MAULIDI KITENGE AUNGANA NA TANESCO KUHAMASISHA NISHATI SAFI YA KUPIKIA KWA UMEME

📌 Aahidi kutumia jukwaa lake kuhamasisha wananchi kutumia umeme kwa shughuli za kupikia 📌 Ushirikiano...

More like this

Sangweni: Sekta ya Mafuta na Gesi Ni Chachu ya Ukuaji wa Uchumi wa Taifa

Na Mwandishi Wetu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli...

VETA Kihonda yaja ‘cold room’ kupunguza upotevu wa mazao ya wakulima

Na Mwandishi Wetu UBUNIFU wa mfumo jumuishi wa kuhifadhi mazao kwa kutumia teknolojia ya ubaridi...

Ofisi ya Msajili wa Hazina yalenga kukusanya Sh2 trilioni mwaka 2026/27

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) imejiwekea lengo la kukusanya Sh2...