PPRA: Mfumo wa NeST utadhibiti rushwa ununuzi wa umma

Na Mwandishi Wetu, Media Brains

MFUMO mpya wa ununuzi wa umma wa kielektroniki unaoitwa National e-Procurement System of Tanzania (NeST), utatarajia kuwa nguzo muhimu ya uwazi na kudhibiti rushwa na usimamizi wa fedha za umma.

Hayo yameelezwa leo Julai 17, 2023 jijini Dodoma na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA), Eliakim Maswi wakati akielezea utekelezaji wa majukumu ya mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa mwaka wa fedha 2023/24.

“Mfumo mpya wa ununuzi kwa njia ya mtandao una lengo la kuhakikisha ununuzi wa umma nchini unazingatia nguzo nne muhimu ambazo ni kuongeza uwazi kwenye ununuzi wa umma, usimamizi mzuri wa fedha za umma, kudhibiti vitendo vya rushwa na ufuatiliaji wa ukidhi wa sheria na uwajibikaji na udhibiti wa ununuzi.

“Kuanzia tarehe 1 Julai 2023, mfumo wa NeST umeanza kutumika rasmi na hii imeenda sambamba na kuzipatia mafunzo taasisi za umma na wazabuni. Kwa mantiki hiyo, taasisi za nunuzi zote ikiwa ni pamoja na wizara, idara za Serikali, taasisi zinazosimiwa na Msajili wa Hazina na Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa,   zinapaswa kuanza  kutumia  mfumo  mpya kwa shughuli za ununuzi wa umma kuanzia mwaka wa fedha 2023/24,” amesema Maswi.

Aidha, ameeleza kuwa kwa takribani miaka minne, Serikali imekuwa ikitumia mfumo wa awali wa TANePS ambao umegubikwa na changamoto mbalimbali baadhi ikiwa ni kutokuwa rafiki kwa watumiaji, kuwa na hitilafu za kiufundi za mara kwa mara na mfumo kuwa na mianya ya kuwezesha taasisi kutotumia mfumo, hivyo kusababisha malalamiko kutoka kwa wazabuni na taasisi.

Pia wazabuni wamekuwa wakilalamika kukosa uwazi, ushindani wa haki, huku kazi na huduma kukosa thamani halisi ya fedha na kuleta malalamiko na hoja nyingi za ukaguzi.

spot_img

Latest articles

YAPO MATAMANIO YA UCHAGUZI WA 2019 KUJIRUDIA 2024?

KUNA uhusiano wowote kati ya mafanikio ya kiuchumi kwa nchi yoyote na kukua kwa...

Dabi ya Kariakoo Wanawake, kitaumana kesho

Na Winfrida Mtoi Mechi ya Dabi ya Kariakoo ya Ligi ya Wanawake Tanzania Bara,...

Baraza la Mawaziri sasa Kidigital- Majaliwa

Na Mwandishi Wetu Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa matumizi ya mfumo wa kielektroniki...

SOMO KUTOKA KWA WATSWANA, WAFUATA NYAYO ZA WAZAMBIA KUING’ARISHA SADC

KUNA habari njema tena kutoka ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)....

More like this

YAPO MATAMANIO YA UCHAGUZI WA 2019 KUJIRUDIA 2024?

KUNA uhusiano wowote kati ya mafanikio ya kiuchumi kwa nchi yoyote na kukua kwa...

Dabi ya Kariakoo Wanawake, kitaumana kesho

Na Winfrida Mtoi Mechi ya Dabi ya Kariakoo ya Ligi ya Wanawake Tanzania Bara,...

Baraza la Mawaziri sasa Kidigital- Majaliwa

Na Mwandishi Wetu Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa matumizi ya mfumo wa kielektroniki...