Zawadi ya gari yawapa mzuka mabondia

Na Winfrida Mtoi

Waandaaji wa pambano la Dar Boxing Derby wameweka gari aina ya Crown ikiwa ni zawadi kwa mshindi kati ya mabondia wa ngumi za kulipwa Tony Rashid na Juma Choki.

Pambano hilo kubwa linatarajiwa kufanyika Julai 24, 2026 jijini Dar es Salaam, huku kila bondia akitamani kuibuka mshindi ili kuondoka na gari hiyo.

“Mimi mwenyewe sina gari, nataka niwe mshindi ili nichukue hili. Nimejipanga vyovyote mpinzani wangu atakavyokuja ndiyo nitakavyocheza kwa kuwa makocha wangu wamemuangalia jinsi anavyocheza”, amesema Tonny Rashid leo Julai 17, 2026 wakati wakizungumza na waandishi wa habari.

Kwa upande wake Juma Choki amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kushudia burudani, kwani pambano lao limepewa thamani kubwa kutokana na zawadi iliyowekwa.

Naye Mratibu wa Matukio kampuni ya Peak Time ambao ni waandaaji wa pambano hilo, Bakari Hatibu amesema lengo la kutoa zawadi licha ya kuwalipa mabondia fedha, ni kuongeza thamani ya mchezo huo.

Sio mara ya kwanza kwa Peak Time kutoa zawadi ya gari kwa mabondia, waliwahi kufanya hivyo kwenye pambano la Dulla Mbabe na Twaha Kiduku ambapo mshindi alikuwa Kiduku.

Mabondia wengine watakaonogesha siku hiyo ni Dulla Mbabe akioneshana ubabe na Hussein Itaba, Haidary Mchanjo na Oscar Richard, wanawake ni Debora mwenda na Dorothea Mhoza, Sara Alex na Dorisia Mazige.

spot_img

Latest articles

MRADI WA UMEME MPOMVU – GGM KUIMARISHA UPATIKANAJI WA UMEME NA KUCHOCHEA SHUGHULI ZA KIUCHUMI GEITA – MHE. SALOME

📌 Kukamilika kwa njia mpya kutatoa fursa kwa njia ya awali kuendelea kunufaisha wananchi...

SERIKALI YAWEKA MKAKATI KUFUFUA SKIMU YA MATIPWILI

Na Mwandishi Wetu SERIKALI imesema iko tayari kufufua na kuboresha skimu ya Umwagiliaji Matipwili...

Tanzania, AngloGold Ashanti kuimarisha ushirikiano

Na Mwandishi Wetu MSAJILI wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amekutana na ujumbe wa kampuni ya...

TANESCO YABAINI MATUKIO YA WIZI WA UMEME KINONDONI KASKAZINI

📌 Operesheni ya ukaguzi wa mita yabaini matumizi yasiyo halali ya umeme eneo la...

More like this