NACTVET yahamasisha elimu ya amali, yataka wazazi kuwapeleka watoto kwenye mafunzo ya ufundi

Na Tatu Mohamed

BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) limewahimiza wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao katika shule zinazotoa elimu ya amali na mafunzo ya ufundi, likisema ndiyo njia ya kuandaa nguvu kazi yenye ujuzi itakayochochea maendeleo ya uchumi wa nchi.

Wito huo umetolewa na Katibu Mtendaji wa NACTVET, Mwajuma Lingwanda, wakati akizungumza katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba), ambapo baraza hilo linaendelea kutoa elimu na huduma mbalimbali kwa wananchi.

Alisema NACTVET imetumia maonesho hayo kusogeza huduma karibu na wananchi kwa kutoa ushauri kuhusu uanzishaji wa taasisi za elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi, pamoja na huduma nyingine zinazopatikana katika ofisi za baraza hilo.

“Tumeridhishwa na mwitikio wa wananchi wanaotembelea banda letu. Wengi wamepata taarifa na huduma walizokuwa wanazihitaji, na tunaamini wataendelea kuwafikishia wengine ujumbe kuhusu fursa zilizopo katika sekta ya elimu ya ufundi,” alisema.

Alibainisha kuwa, moja ya vivutio vikubwa katika banda la NACTVET mwaka huu ni ushiriki wa wanafunzi wa shule za amali wanaoonesha kwa vitendo ujuzi walioupata darasani kupitia kazi mbalimbali wanazozifanya.

Alisema maonesho hayo yanadhihirisha kuwa wanafunzi hao wanapata maarifa ya vitendo yanayowawezesha kuingia moja kwa moja kwenye soko la ajira au kujiajiri mara baada ya kuhitimu masomo yao.

“Hawa vijana wanaonesha uwezo wao kutokana na mafunzo waliyopata. Hii ni ishara kuwa elimu ya amali inawajengea uwezo wa kufanya kazi na kuzalisha mara tu wanapomaliza masomo,” alisema.

Aliongeza kuwa mafunzo ya ufundi na elimu ya amali yana mchango mkubwa katika kuzalisha wataalamu wenye ujuzi wa kujiajiri, kuajiriwa, kubuni teknolojia na kuongeza thamani ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa nchini.

Hata hivyo, aliwahimiza wawekezaji na wadau wa elimu kutumia fursa zilizopo kuanzisha shule na taasisi zinazotoa mafunzo ya amali na ufundi stadi, akisema NACTVET ipo tayari kutoa ushauri na kuelekeza taratibu zote zinazohitajika.

Akizungumzia mchango wa sekta hiyo katika maendeleo ya taifa, alisema elimu ya ufundi na mafunzo ya amali ni nyenzo muhimu ya kufanikisha Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kwa kuwa inajenga nguvu kazi yenye ujuzi, inayochochea uzalishaji, ubunifu, biashara na ukuaji wa viwanda.

Alisema uwepo wa bidhaa nyingi zinazozalishwa nchini na kuoneshwa katika Maonesho ya Sabasaba unaashiria kuwa Tanzania inaendelea kujenga uchumi unaotegemea uzalishaji na ujuzi wa Watanzania, hali inayochangia kuongeza ajira na kuimarisha maendeleo ya Taifa.

spot_img

Latest articles

GCLA yatumia Sabasaba kutoa elimu ya usalama wa kemikali na huduma za maabara

Na Mwandishi Wetu Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) imesema imejipanga kutumia...

WANANCHI WAHAMASISHWA KUTUMIA UMEME KATIKA VYOMBO VYA USAFIRI ILI KUPUNGUZA GHARAMA ZA USAFIRI

📌 TANESCO yaeleza matumizi ya umeme katika magari, bajaji na pikipiki 📌 Pikipiki ya umeme...

TTB YAMKABIDHI KHALID AL BARWANI UBALOZI WA HIARI WA UTALII KUITANGAZA TANZANIA DUNIANI

Na Mwandishi Wetu BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imemkabidhi rasmi mwanautalii na mtangazaji wa...

Serikali yaongeza msukumo wa kuwajengea vijana ujuzi unaokidhi soko la ajira

Na Mwandishi Wetu Serikali imesema itaendelea kuwekeza katika programu za kuwawezesha vijana kupata ujuzi...

More like this

GCLA yatumia Sabasaba kutoa elimu ya usalama wa kemikali na huduma za maabara

Na Mwandishi Wetu Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) imesema imejipanga kutumia...

WANANCHI WAHAMASISHWA KUTUMIA UMEME KATIKA VYOMBO VYA USAFIRI ILI KUPUNGUZA GHARAMA ZA USAFIRI

📌 TANESCO yaeleza matumizi ya umeme katika magari, bajaji na pikipiki 📌 Pikipiki ya umeme...

TTB YAMKABIDHI KHALID AL BARWANI UBALOZI WA HIARI WA UTALII KUITANGAZA TANZANIA DUNIANI

Na Mwandishi Wetu BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imemkabidhi rasmi mwanautalii na mtangazaji wa...