TPDC Yapanua Matumizi ya Gesi Asilia, Yaweka Mkazo Kwa Nishati ya Kupikia

Na Tatu Mohamed

SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limesema linaendelea na jitihada za kuongeza matumizi ya gesi asilia nchini, hususan katika sekta ya kupikia, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuwafikia wananchi wengi zaidi na kuwawezesha kutumia nishati safi na salama.

Akizungumza katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), Afisa Masoko wa TPDC, Neema Cleophace, alisema gesi asilia inayotumika nchini inapatikana katika mikoa ya Mtwara na Lindi na ina matumizi mbalimbali ikiwemo majumbani, kwenye magari, viwandani na katika uzalishaji wa umeme.

Alisema takribani asilimia 70 ya gesi asilia inayozalishwa nchini hutumika kuzalisha umeme, huku TPDC ikiwa tayari imeunganisha zaidi ya nyumba 2,500 kutumia gesi asilia kwa matumizi ya majumbani.

“Matumizi ya gesi asilia kwenye sekta ya usafiri nayo yanaendelea kukua ambapo zaidi ya magari 5,000 tayari yanatumia nishati hii, yakihudumiwa na vituo zaidi ya 18 vya kujazia gesi asilia vilivyopo nchini,” alisema.

Aidha, alisema zaidi ya viwanda 59 nchini vinatumia gesi asilia katika shughuli zao za uzalishaji kutokana na faida zake za kupunguza gharama za nishati na kuongeza ufanisi wa uzalishaji.

Akizungumzia mipango ya mwaka huu wa fedha, alisema TPDC imejipanga kuongeza idadi ya nyumba zitakazounganishwa na huduma ya gesi asilia kwa ajili ya kupikia.

“Kwa Dar es Salaam tunatarajia kuunganisha zaidi ya nyumba 1,000. Pia tuna mpango wa kuunganisha zaidi ya nyumba 800 katika Wilaya ya Mkuranga na zaidi ya nyumba 800 katika Mkoa wa Mtwara,” alisema.

Alitoa wito kwa wananchi kutembelea banda la TPDC katika Maonesho ya Sabasaba ili kujifunza kuhusu shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na shirika hilo, pamoja na kupata elimu kuhusu matumizi na faida za gesi asilia katika maisha ya kila siku.

“TPDC itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha matumizi ya gesi asilia yanaongezeka nchini, hatua ambayo itachangia upatikanaji wa nishati safi, salama na yenye gharama nafuu kwa wananchi na sekta za uzalishaji,” alisisitiza.

spot_img

Latest articles

TTB yatumia Sabasaba kuitangaza SITE 2026

Na Tatu Mohamed BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imesema imeanzisha dawati maalumu katika Maonesho...

TTCL yaahidi kuimarisha huduma za kidijitali nchini

Na Tatu Mohamed SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limesema litaendelea kuimarisha huduma za mawasiliano nchini...

TANZANIA NA URUSI ZAIMARISHA USHIRIKIANO WA UTALII KUPITIA MAKUBALIANO MAPYA

Na Mwandishi Wetu TANZANIA na Urusi zimesaini Hati ya Makubaliano (MoU) ya ushirikiano katika...

TANESCO yazindua Nyumba Janja, yatoa majiko ya umeme kwa mkopo Sabasaba

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limezindua Nyumba Janja yenye...

More like this

TTB yatumia Sabasaba kuitangaza SITE 2026

Na Tatu Mohamed BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imesema imeanzisha dawati maalumu katika Maonesho...

TTCL yaahidi kuimarisha huduma za kidijitali nchini

Na Tatu Mohamed SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limesema litaendelea kuimarisha huduma za mawasiliano nchini...

TANZANIA NA URUSI ZAIMARISHA USHIRIKIANO WA UTALII KUPITIA MAKUBALIANO MAPYA

Na Mwandishi Wetu TANZANIA na Urusi zimesaini Hati ya Makubaliano (MoU) ya ushirikiano katika...