TTB yatumia Sabasaba kuitangaza SITE 2026

Na Tatu Mohamed

BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imesema imeanzisha dawati maalumu katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi na wadau kuhusu Maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya Swahili International Tourism Expo (SITE) 2026.

Akizungumza katika maonesho hayo, Afisa Masoko wa TTB, Abdilahi Ameir, alisema dawati hilo linatumika kuhamasisha wananchi na wadau kushiriki maonesho ya SITE pamoja na kuwafahamisha kuhusu fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya utalii.

Amesema SITE ni maonesho ya kimataifa yanayowakutanisha wadau wa biashara ya utalii na wanunuzi wa huduma za utalii kutoka mataifa mbalimbali duniani kwa lengo la kukuza biashara na kuitangaza Tanzania kama kitovu cha utalii.

Kwa mujibu wa Ameir, maandalizi ya SITE 2026 yanaendelea vizuri, huku zaidi ya wanunuzi 50 wa huduma za utalii kutoka nchi mbalimbali, ikiwemo Korea, Urusi na nchi za Ulaya Mashariki, wakiwa tayari wamethibitisha ushiriki wao.

Aidha, alisema wananchi wa kawaida hawajaachwa nyuma kwani kutakuwa na bustani maalumu ya wanyama pori itakayowapa fursa ya kujifunza na kujionea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

Ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki Maonesho ya Swahili International Tourism Expo yatakayofanyika kuanzia Julai 23 hadi 25 katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, ili kujionea fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji katika sekta ya utalii.

spot_img

Latest articles

JAB yazindua mwongozo wa kisheria wa utoaji wa Ithibati ya maisha kwa waandishi

Na Mwandishi Wetu BODI ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imezindua rasmi Mwongozo wa...

BRELA YAIBUA FURSA MPYA ULINZI WA ALAMA ZA BIASHARA KWA WAJASIRIAMALI

Na Mwandishi Wetu Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imewataka wajasiriamali wanaoshiriki...

TTB yakutanisha wadau kujadili mustakabali wa Destination Tanzania

Na Mwandishi Wetu Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imewakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya...

Dkt. Jafar Seif: Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu Sabasaba larahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi

Na Mwandishi Wetu NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za...

More like this