TANZANIA NA URUSI ZAIMARISHA USHIRIKIANO WA UTALII KUPITIA MAKUBALIANO MAPYA

Na Mwandishi Wetu

TANZANIA na Urusi zimesaini Hati ya Makubaliano (MoU) ya ushirikiano katika sekta ya utalii, hatua inayolenga kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili na kuongeza fursa za utalii, biashara na uwekezaji.

Makubaliano hayo yanaenda sambamba na kuanza kwa safari za moja kwa moja za kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) zinazounganisha Moscow na Tanzania Bara pamoja na Zanzibar, hatua itakayorahisisha usafiri wa watalii na wafanyabiashara kati ya masoko hayo mawili.

Katika safari hiyo ya kihistoria ya kwanza, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kijaji, aliongoza ujumbe wa Tanzania uliojumuisha Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) pamoja na wadau zaidi ya kampuni 47 za utalii.Ujumbe huo ulikutana na wadau wa sekta ya utalii kutoka Urusi kupitia mikutano ya biashara baina ya wafanyabiashara (B2B), iliyowapa fursa ya kujadiliana, kujenga ushirikiano mpya wa kibiashara na kutangaza vivutio vya kipekee vya utalii vya Tanzania kwa soko la Urusi.

Hatua hii inatarajiwa kuongeza idadi ya watalii kutoka Urusi, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika sekta ya utalii, na kuchangia utekelezaji wa malengo ya Tanzania ya kukuza sekta ya utalii na uchumi wa nchi kupitia masoko mapya ya kimkakati.

spot_img

Latest articles

JAB yazindua mwongozo wa kisheria wa utoaji wa Ithibati ya maisha kwa waandishi

Na Mwandishi Wetu BODI ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imezindua rasmi Mwongozo wa...

BRELA YAIBUA FURSA MPYA ULINZI WA ALAMA ZA BIASHARA KWA WAJASIRIAMALI

Na Mwandishi Wetu Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imewataka wajasiriamali wanaoshiriki...

TTB yakutanisha wadau kujadili mustakabali wa Destination Tanzania

Na Mwandishi Wetu Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imewakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya...

Dkt. Jafar Seif: Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu Sabasaba larahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi

Na Mwandishi Wetu NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za...

More like this