Ofisi ya Usuluhishi wa Kodi Yaahidi Kuimarisha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji

Na Mwandishi Wetu

OFISI ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi imesema, inaendelea kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini kwa kushughulikia malalamiko ya walipakodi, hatua inayolenga kuongeza ulipaji wa kodi kwa hiari na kuchangia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Akizungumza katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba), Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi, Erastus Mtui amesema taasisi hiyo, ambayo imeanza rasmi shughuli zake takribani miaka miwili na nusu iliyopita, inatumia maonesho hayo kutoa elimu kwa wananchi kuhusu majukumu yake pamoja na kupokea malalamiko na taarifa za kodi.

Amesema moja ya malengo ya kuanzishwa kwa ofisi hiyo ni kuhakikisha mfanyabiashara na mwekezaji anapokutana na changamoto za kikodi anakuwa na sehemu ya kuwasilisha malalamiko yake ili yapatiwe ufumbuzi.

“Kodi ni jambo muhimu katika uendeshaji wa nchi. Tunawahimiza walipakodi walipe kodi zao kwa hiari, na pale wanapokutana na kikwazo, sisi tupo kwa ajili ya kukiondoa ili waweze kutimiza wajibu wao kwa urahisi,” amesema.

Amesema ofisi hiyo ina nafasi muhimu katika kufanikisha Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kwa kuwa mazingira bora ya biashara na uwekezaji ni msingi wa kukuza uchumi unaolengwa kufikia wastani wa ukuaji usiopungua asilimia 10 na kuelekea uchumi wa dola trilioni moja.

Amefafanua kuwa jukumu la ofisi hiyo ni kushughulikia changamoto za kikodi kwa wakati ili kuondoa vikwazo vinavyoweza kuathiri ukuaji wa biashara na uwekezaji.

Aidha, amesema wananchi wanaweza kuwasilisha malalamiko yao kwa kufika ofisini, kupitia simu za bure, mfumo wa mtandao pamoja na programu ya Suluhu ya Kodi App kwa watumiaji wa simu janja.

Ameongeza kuwa ofisi hiyo imekamilisha maandalizi ya mfumo wa USSD utakaowawezesha pia wananchi wanaotumia simu zisizo janja kuwasilisha malalamiko yao kwa urahisi.

Akizungumzia mafanikio ya taasisi hiyo, amesema katika kipindi cha miaka miwili na nusu tangu kuanzishwa kwake, ofisi imepokea na kushughulikia malalamiko 593, huku malalamiko 340 yakishughulikiwa katika mwaka uliopita pekee.

Amewataka wananchi kutembelea banda la Ofisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi katika Maonesho ya Sabasaba ili kupata elimu kuhusu huduma zinazotolewa na namna ya kuwasilisha malalamiko yanayohusiana na kodi.

spot_img

Latest articles

TTCL Yakabidhi Magari 6 ya Sh. Milioni 903 Kuimarisha Ufanisi wa Huduma

Na Mwandishi Wetu SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeendelea kutekeleza mkakati wake wa kuboresha...

Mkondo wa amali waanza kuzaa matunda, wanafunzi waonesha ubunifu Sabasaba

Na Tatu Mohamed WANAFUNZI wanaosoma mkondo wa amali wameanza kuonesha matokeo ya ujuzi wa...

NAIBU GAVANA WA BoT ATEMBELEA BANDA LA BODI YA BIMA YA AMANA MAONESHO YA SABASABA DAR ES SALAAM

Na Mwandishi Wetu NAIBU Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Rahma Salim...

Waziri Katambi anatengeneza janga kubwa

MEI mwaka huu picha mjongeo ya mahojiano kati ya Inspekta Jenerali wa Polisi Mstaafu,...

More like this

TTCL Yakabidhi Magari 6 ya Sh. Milioni 903 Kuimarisha Ufanisi wa Huduma

Na Mwandishi Wetu SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeendelea kutekeleza mkakati wake wa kuboresha...

Mkondo wa amali waanza kuzaa matunda, wanafunzi waonesha ubunifu Sabasaba

Na Tatu Mohamed WANAFUNZI wanaosoma mkondo wa amali wameanza kuonesha matokeo ya ujuzi wa...

NAIBU GAVANA WA BoT ATEMBELEA BANDA LA BODI YA BIMA YA AMANA MAONESHO YA SABASABA DAR ES SALAAM

Na Mwandishi Wetu NAIBU Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Rahma Salim...