Msaidizi wa Lissu apatikana na pingu mkononi, aeleza kilichomkuta

Na Mwandishi Wetu

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Bara, Amani Golugwa, amesema David Jumbe, msaidizi wa Mwenyekiti wa Chama hicho, Tundu Lissu amepatikana akiwa na pingu mkononi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Mei 21, 2026, Golugwa amethibitisha Jumbe kuchukuliwa usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake.

 “Asubuhi hii familia, mke wake amenijulisha kwamba Jumbe amepatikana akiwa katika hali mbaya sana akiwa na pingu mkononi, tunawaambia Polisi Jumbe yupo nyumbani kwake waende kumfungulia pingu,” amesema.

Alieleza kuwa Golugwa Polisi walifika makao makuu ya Chadema leo Alhamisi, Mei 21, 2026 saa tatu asubuhi walijitambulisha wanatoka kituo cha Polisi Oysterbay na wanamtafuta Jumbe ambaye walidai alitoweka na pingu.

Baada ya kupatikana, Jumbe amezungumza kupitia video iliyowekwa kwenye mitandao ya kijamii ya Chadema amesema alichukuliwa akiwa anarejea nyumbani akitokea katika shughuli zake za kila siku.

“Majira ya saa nne kasoro nilikuwa natoka kwenye shughuli zangu narejejea nyumbani nikiwa na jirani yangu, rafiki yangu, nilikuwa natumia gari yake, mimi naendesha yeye amekaa upande wa pili, wakati tumekaribia kabisa nyumbani kwangu gari imekuja ikapita kulia kwangu, ikaniblock kwa mbele, alafu na nyingine kwa nyuma.

“Wakashuka watu wengi kama watano au sita wakafungua mlango wangu wakamshusha yule bwana niliyekuwa naye upande wa pili, wakambeba kwa nguvu na mimi nikajua ni utekaji nikaanza kupambana nao napiga kelele, watekaji watekaji. Nikaanza kupambana nao kwa kupiga ngumi lakini wakaja wengi wakanizidi nguvu, wakanirusha nyuma ya ile gari, kunifunga pingu na kuanza kunishambulia,” ameeleza Jumbe.

Awali, taarifa za kutoweka kwa Jumbe zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa alichukuliwa nyumbani kwake Mabwepande, Bunju jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo na watu wasiojulikana.

Kauli ya Jeshi la Polisi

spot_img

Latest articles

Tanesco yaendelea kuwaelimisha wanaofanya shughuli za kiuchumi kwenye miundombinu ya umeme

📌Ni katika muendelezo wa ukaguzi wa miundombinu ya umeme Dar es salaam 📌Yatoa rai kwa...

‎DAWASA yapeleka agenda ya kudhibiti upotevu wa maji Pwani

Na Mwandishi Wetu MAPAMBANO dhidi ya upotevu wa maji yamepokelewa vyema na uongozi wa...

Tanzania yataka ushirikiano imara na kuvuka mipaka kutokomeza maralia 

Na John Mapepele, Geneva, Uswisi  WAZIRI wa Afya wa Tanzania, Mohamed Mchengerwa, ametoa wito wa...

Ofisi ya Msajili wa Hazina yaendesha mafunzo ya Usimamizi wa vihatarishi kwa Taasisi za Umma

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OMH), kupitia Kitengo cha usimamizi wa...

More like this