Sowah apigwa faini nzito  kwa utovu wa nidhamu, ashushwa U-20

Na Winfrida Mtoi

UONGOZI wa Klabu ya Simba umeweka wazi hatua kali za kinidhamu zilizochukuliwa dhidi ya mshambuliaji wao, Jonathan Sowah, ikiwemo kuondolewa kwenye kikosi cha wakubwa na kutakiwa kufanya mazoezi na timu ya vijana (U-20).

​Hatua hiyo imekuja kufuatia malalamiko mfululizo kutoka kwa Benchi la Ufundi la klabu hiyo, yaliyomtuhumu mchezaji huyo kwa makosa mbalimbali ya utovu wa nidhamu.

​Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amefafanua leo Aprili 14, 2026, kuwa sakata hilo lilianza kushika kasi mwezi Machi wakati timu hiyo ilipokuwa safarini jijini Dodoma.

​”Mwezi wa tatu tulipokuwa Dodoma kwa ajili ya mchezo dhidi ya Dodoma Jiji, Sowah aliamrishwa kuondoka kambini na kurejea Dar es Salaam mara moja kutokana na tuhuma za utovu wa nidhamu zilizowasilishwa na benchi la ufundi.

“​Baada ya kurejeshwa Dar es Salaam, Sowah alifikishwa mbele ya Kamati ya Nidhamu ya klabu ambapo alisomewa mashtaka yake na  mchezaji huyo alikiri baadhi ya makosa na kutoa maelezo kwa mengine.

​Amesema  kamati ilijiridhisha na makosa yake na kutoa adhabu mbili ya  kulipa faini na kufanya mazoezi na timu ya vijana (U-20).

​Uongozi umesisitiza kuwa adhabu ya kumshusha Sowah kwenye timu ya vijana si ya kudumu, bali ni kipindi cha mpito cha kumfanyia tathmini.

​”Adhabu ya kufanya mazoezi na vijana inalenga kumpa nafasi ya kujitathmini na kuonyesha mabadiliko. Tukijiridhisha kuwa amebadilika, basi atarejeshwa kwenye kikosi cha wakubwa kuendelea na majukumu yake,” alihitimisha Meneja huyo.

spot_img

Latest articles

Rais Mwinyi akagua Mji wa AFCON Fumba

Na Mwandishi WetuRAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali...

Waziri Mavunde aelekeza kusimamishwa kwa shughuli za uchimbaji Busulwangili-Kahama – Kahama

Na Mwandishi wetu, Dodoma WAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde, ameagiza kusimamishwa mara moja kwa...

DC Mkude akabidhi vyombo vya usafiri Tanesco Mkoa wa Arusha kuimarisha utoaji huduma

📌 Ni katika muendelezo wa mkakati wa TANESCO wa kuwahudumia wananchi kwa ufanisi zaidi. 📌...

DCEA yakamata Kilo 101.2 za Mirungi ndani ya Basi la Abood, watano mbaroni

Na Mwandishi wetu Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imekamata...

More like this