Vita ya kusaka tiketi ya China 2026 yanoga, Waogeleaji 200 wachuana vikali

Na Winfrida Mtoi

IKIWA ni siku ya pili ya Mashindano ya Taifa ya mchezo wa kuogelea,   waogeleaji  wa klabu mbalimbali wameendelea kuchuana vikali kufatuta rekodi mpya, huku  rekodi zikiendelea kuvunjwa.

Miongoni mwa waogeleaji waliofanikiwa kuvunja rekodi katika mashindano hayo ni Crissa Dillip  kutoka klabu ya Tallis aliyevunja rekodi ya mita 100 free style kwa wasichana.

Mashindano hayo yanayofanyika katika bwawa la kuogelea la kuogelea la Shule ya Kimataifa ya Tanganyika(IST), Masaki, jijini Dar es Salaam, yanashirikisha waogeleaji 200 kutoka klabu 16.

Bila kujali hali ya hewa ya mvua katika mashindano hayo, ushindani  ni mkali kutokana na uwezo wa washiriki, huku kila mmoja akitamani kuvunja rekodi.

Akizungumzia mashindano hayo, Mwenyekiti wa Chama cha Mchezo wa Kuogelea  Tanzania (TSA), David Mwansyoge amesema  mashindano yamezingatia vigezo vya hali ya juu kwa sababu yanatumika  kufuzu Mashindano ya Dunia ya Kuogelea (World Aquatics Short Course Championship) yatakayofanyika nchini China Desemba 2026.

“Jana tulianza na umbali mrefu mita 800, tukiamini kwamba umbali mrefu ni eneo ambalo tunaweza kufanya vizuri zaidi katika muda mfupi.Tumeona rekodi zikivunjwa na tunategemea rekodi nyingi kuvunjwa kwa kuwa ushindani ni mkubwa,” ameeleza Mwansyoge.

Kwa upande wake Crissa akielezea  ubora wake  anasema ni kutokana na sapoti anayopa kuanzia kwa wazazi wake, huku akiwataka wasichana kujitokeza katika mchezo huo.

spot_img

Latest articles

Mchezo wa kuogelea wazidi kupaa nchini, TSA  yafichua siri

Na Winfrida  Mtoi MCHEZO wa kuogelea umezidi kushika kasi nchini  kutokana na kuongezeka idadi ya...

Dkt Nchimbi atembelea banda la Tanesco

Na Mwandishi Wetu MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi...

Waogeleaji chipukizi 400 kutikisa Dar kesho

Na Mwandishi Wetu Zaidi ya waogeleaji 400 wenye umri wa miaka 6 hadi 12 wanatarajiwa...

Wabunge walifuata mkumbo kwenda Morocco kuishangilia Serengeti Boys lawakuta jambo

Na Mwandishi Wetu SPIKA wa Mbunge la Tanzania, Mussa Azzan Zungu ametoa siku nne za...

More like this

Mchezo wa kuogelea wazidi kupaa nchini, TSA  yafichua siri

Na Winfrida  Mtoi MCHEZO wa kuogelea umezidi kushika kasi nchini  kutokana na kuongezeka idadi ya...

Dkt Nchimbi atembelea banda la Tanesco

Na Mwandishi Wetu MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi...

Waogeleaji chipukizi 400 kutikisa Dar kesho

Na Mwandishi Wetu Zaidi ya waogeleaji 400 wenye umri wa miaka 6 hadi 12 wanatarajiwa...